07-Imaam An-Nawawiy: Kula Kusudi Na Kujamiana Mchana Wa Ramadhwaan

Kula Kusudi Na Kujamiana Mchana Wa Ramadhwaan

 

Imaam An-Nawawiy (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, mtu ambaye anakula kwa kukusudia mchana wa Ramadhwaan ni waajib kwake kulipa kaffaarah? 

 

Je, mtu ambaye kwa kusudi anamuingilia mke wake mchana wa Ramadhwaan alipe kafara? Na kama alimuingilia mara kadhaa wakati wa Ramadhwaan, anapaswa kulipa kaffaraah mara kadhaa?

 

 

JIBU:

 

Kuhusiana na kafara (ya kula kwa makusudi mchana wa Ramadhwaan) halazimiki kulipa kafara. Hata hivyo anapata madhambi na analazimika kulipa siku iliyobaki. Hali kadhalika anapaswa kulipa siku alizofanya hivyo na kufanya tawbah.

 

Ama kuhusiana masuala ya kumuingilia mke, analazimika kulipa kafara kwa ile mara ya kwanza ya kumuingia mke na si lazima kwa kila mara (kwa siku hiyo aliyofanya tendo hilo).  

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

[Imaam Abuu Zakariyyah An-Nawawiy - Fataawaa  Imaam An-Nawawiy, uk. 55]

Share