01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Al-Huduwd (Adhabu): Mlango Wa Adhabu Ya Uzinifu

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْحُدُودِ

Kitabu Cha Al-Huduwd (Adhabu)[1]

 

بَابُ حَدِّ اَلزَّانِي

01-Mlango Wa Adhabu Ya Uzinifu

 

 

 

 

 

1033.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ وَزَيْدِ بْنِ خَالِدٍ اَلْجُهَنِيِّ رَضِيَ اَللَّهُ عنهما {أَنَّ رَجُلًا مِنَ اَلْأَعْرَابِ أَتَى رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! أَنْشُدُكَ بِاَللَّهِ إِلَّا قَضَيْتَ لِي بِكِتَابِ اَللَّهِ، فَقَالَ اَلْآخَرُ ‏ وَهُوَ أَفْقَهُ مِنْهُ ‏ نَعَمْ.‏ فَاقَضِ بَيْنَنَا بِكِتَابِ اَللَّهِ، وَأْذَنْ لِي، فَقَالَ: "قُلْ".‏ قَالَ: إنَّ اِبْنِي كَانَ عَسِيفًا عَلَى هَذَا فَزَنَى بِاِمْرَأَتِهِ، وَإِنِّي أُخْبِرْتُ أَنْ عَلَى اِبْنِي اَلرَّجْمَ، فَافْتَدَيْتُ مِنْهُ بِمَائَةِ شَاةٍ وَوَلِيدَةٍ، فَسَأَلَتُ أَهْلَ اَلْعِلْمِ، فَأَخْبَرُونِي: أَنَّمَا عَلَى اِبْنِيْ جَلْدُ مَائَةٍ وَتَغْرِيبُ عَامٍ، وَأَنَّ عَلَى اِمْرَأَةِ هَذَا اَلرَّجْمَ، فَقَالَ رَسُولُ ا للَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏"وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَأَقْضِيَنَّ بَيْنَكُمَا بِكِتَابِ اَللَّهِ، اَلْوَلِيدَةُ وَالْغَنَمُ رَدٌّ عَلَيْكَ، وَعَلَى اِبْنِكَ جَلْدُ مِائَةٍ وَتَغْرِيبُ عَامٍ، وَاغْدُ يَا أُنَيْسُ إِلَى اِمْرَأَةِ هَذَا، فَإِنْ اِعْتَرَفَتْ فَارْجُمْهَا"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، هَذَا وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah na Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) wamesema: Mtu mmoja katika mabedui alimjia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Nakuomba kwa Allaah unihukumu kwa Kitabu Cha Allaah”. Mwingine ambaye ni mjuzi kuliko yeye akasema: “Ndio, hukumu baina yetu kwa Kitabu Cha Allaah, na uniruhusu niseme.” Akasema Rasuli wa Allaah: “Sema.” Akasema: “Mwanangu alikuwa ni muajiriwa wa huyu, akazini na mkewe, nami nilikuwa nimeambiwa kuwa mwanangu atarujumiwa, nimemtolea fidia ya mbuzi mia na mjakazi. Nikawauliza wenye ilmu wakaniambia kuwa mwanangu achapwe mijeledi mia na atolewe mjini mwaka mmoja na mke wa huyu arujumiwe. Akasema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ):  “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi mwake! Nitahukumu baina yenu kwa Kitabu Cha Allaah. Mjakazi na mbuzi warudishwe kwako. Na mwanao achapwe mijeledi mia na kutolewa mjini mwaka mmoja. Ee Unays, nenda hadi kwa mke wa bwana huyu, akiungama umrajimu (umpige mawe).”[2] [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

1034.

وَعَنْ عُبَادَةَ بْنِ اَلصَّامِتِ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{خُذُوا عَنِّي، خُذُوا عَنِّي، فَقَدْ جَعَلَ اَللَّهُ لَهُنَّ سَبِيلاً، اَلْبِكْرُ بِالْبِكْرِ جَلْدُ مِائَةٍ، وَنَفْيُ سَنَةٍ، وَالثَّيِّبُ بِالثَّيِّبِ جَلْدُ مِائَةٍ، وَالرَّجْمُ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ.‏

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Chukueni kutoka kwangu, chukueni kutoka kwangu. Allaah Amewajaalia (wanawake) kupata njia.[3] Mume asiye na mke, na mke asiye na mume (watakapozini) watapigwa mijeledi mia na kutolewa mjini mwaka mmoja. Mume aliyeowa na mke aliyeolewa (wakizini) watapigwa mijeledi mia[4] na kupigwa mawe (Rajm).” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1035.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ قَالَ: {أَتَى رَجُلٌ مِنْ اَلْمُسْلِمِينَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏‏وَهُوَ فِي اَلْمَسْجِدِ‏ فَنَادَاهُ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي زَنَيْتُ، فَأَعْرَضَ عَنْهُ، فَتَنَحَّى تِلْقَاءَ وَجْهِهِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي زَنَيْتُ، فَأَعْرَضَ عَنْهُ، حَتَّى ثَنَّى ذَلِكَ عَلَيْهِ أَرْبَعَ مَرَّاتٍ، فَلَمَّا شَهِدَ عَلَى.‏ نَفْسِهِ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ.‏ دَعَاهُ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏فَقَالَ "أَبِكَ جُنُونٌ ؟" قَالَ.‏ لَا.‏ قَالَ: "فَهَلْ أَحْصَنْتَ ؟".‏ قَالَ: نَعَمْ.‏ فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏"اِذْهَبُوا بِهِ فَارْجُمُوهُ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Mtu mmoja katika Waislamu alimjia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa Msikitini, akamnadia: “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nimezini.” Rasuli wa Allaah akampa mgongo, akamuendea akamuambia: “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nimezini!” Rasuli wa Allaah akampa mgongo, hata akaikariri kauli hiyo mara nne. Alipojishuhudia zinaa yeye mwenyewe mara nne, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimuita akamuuliza: “Una wazimu?” Akasema: “Laa (hapana).” Akasema: “Umehifadhika (una mke)?” Akasema: “Ndio.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Mchukueni na mumrajimu.”[5] [Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1036.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {لَمَّا أَتَى مَاعِزُ بْنُ مَالِكٍ إِلَى اَلنَّبِيِّ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏قَالَ لَهُ: "لَعَلَّكَ قَبَّلْتَ، أَوْ غَمَزْتَ، أَوْ نَظَرْتَ ؟" قَالَ: لَا يَا رَسُولَ اَللَّهِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Maa’iz bin Maalik alipokuja kwa Nabiy[6] (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Pengine ulibusu au uligusa au ulitazama.” Akasema Maa’iz: “Sivyo Ee Rasuli wa Allaah!” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1037.

وَعَنْ عُمَرَ بْنِ اَلْخَطَّابِ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ {أَنَّهُ خَطَبَ فَقَالَ: إِنَّ اَللَّهَ بَعَثَ مُحَمَّدًا بِالْحَقِّ، وَأَنْزَلَ عَلَيْهِ اَلْكِتَابَ، فَكَانَ فِيمَا أَنْزَلَ اَللَّهُ عَلَيْهِ آيَةُ اَلرَّجْمِ.‏ قَرَأْنَاهَا وَوَعَيْنَاهَا وَعَقَلْنَاهَا، فَرَجَمَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏وَرَجَمْنَا بَعْدَهُ، فَأَخْشَى إِنْ طَالَ بِالنَّاسِ زَمَانٌ أَنْ يَقُولَ قَائِلٌ: مَا نَجِدُ اَلرَّجْمَ فِي كِتَابِ اَللَّهِ، فَيَضِلُّوا ‏ بِتَرْكِ فَرِيضَةٍ أَنْزَلَهَا اَللَّهُ، وَإِنَّ اَلرَّجْمَ حَقٌّ فِي كِتَابِ اَللَّهِ عَلَى مَنْ زَنَى، إِذَا أُحْصِنَ مِنْ اَلرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ، إِذَا قَامَتْ اَلْبَيِّنَةُ، أَوْ كَانَ اَلْحَبَلُ، أَوْ اَلِاعْتِرَافُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alihutubia akasema: “Kwa hakika Allaah Alimtuma Muhammad (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kwa haki, Akamteremshia Kitabu, ikawa katika Aliyomteremshia ni Aayah ya Rajmi, tuliisoma tukaihifadhi na tukaizingatia. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akapiga kwa mawe (Rajm), na sisi baada yake tukapiga kwa mawe. Kwa hivyo nachelea isije zama zikawa ndefu kwa watu akaja kusema mwenye kusema: “Mbona hatuoni kupiga kwa mawe (Rajm) katika Kitabu Cha Allaah!” Kwa ajili hiyo wakapotea kwa kuacha faradhi Aliyoiteremsha Allaah. Na kwa hakika Rajm kumethubutu katika Kitabu Cha Allaah[7] kwa mwenye kuzini aliyeoa au ameolewa miongoni mwa wanaume na wanawake utakaposimama ubainifu au kwa kushika mimba au kwa kukiri.” [Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1038.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏يَقُولُ: {"إِذَا زَنَتْ أَمَةُ أَحَدِكُمْ، فَتَبَيَّنَ زِنَاهَا، فَلْيَجْلِدْهَا اَلْحَدَّ، وَلَا يُثَرِّبْ عَلَيْهَا، ثُمَّ إِنْ زَنَتْ فَلْيَجْلِدْهَا اَلْحَدَّ، وَلَا يُثَرِّبْ عَلَيْهَا، ثُمَّ إِنْ زَنَتِ اَلثَّالِثَةَ، فَتَبَيَّنَ زِنَاهَا، فَلْيَبِعْهَا وَلَوْ بِحَبْلٍ مِنْ شَعَرٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِمٍ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Atakapozini mjakazi wa mmoja wenu[8] na uzinifu wake ukabainika, basi ampe adhabu kwa kumchapa mijeledi wala asimkaripie. Atakapozini tena amchape mijeledi wala asimkaripie. Atakapozini mara ya tatu uzinifu wake ukabainika basi amuuze japo kwa kamba ya nywele.” [Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

1039.

وَعَنْ عَلِيٍّ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{أَقِيمُوا اَلْحُدُودَ عَلَى مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wasimamishieni adhabu iliyowamiliki mikono yenu.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

 

 

1040.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حَصِينٍ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ {أَنَّ اِمْرَأَةً مِنْ جُهَيْنَةَ أَتَتْ نَبِيَّ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏‏وَهِيَ حُبْلَى مِنْ اَلزِّنَا‏فَقَالَتْ: يَا نَبِيَّ اَللَّهِ! أَصَبْتُ حَدًّا، فَأَقِمْهُ عَلَيَّ، فَدَعَا نَبِيُّ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏وَلِيَّهَا.‏ فَقَالَ: "أَحْسِنْ إِلَيْهَا فَإِذَا وَضَعَتْ فَائْتِنِي بِهَا" فَفَعَلَ.‏ فَأَمَرَ بِهَا فَشُكَّتْ عَلَيْهَا ثِيَابُهَا، ثُمَّ أَمَرَ بِهَا فَرُجِمَتْ، ثُمَّ صَلَّى عَلَيْهَا، فَقَالَ عُمَرُ: أَتُصَلِّي عَلَيْهَا يَا نَبِيَّ اَللَّهِ وَقَدْ زَنَتْ ؟ فَقَالَ: "لَقَدْ تَابَتْ تَوْبَةً لَوْ قُسِّمَتْ بَيْنَ سَبْعِينَ مِنْ أَهْلِ اَلْمَدِينَةِ لَوَسِعَتْهُمْ، وَهَلْ وَجَدَتْ أَفَضَلَ مِنْ أَنْ جَادَتْ بِنَفْسِهَا لِلَّهِ ؟} ".‏ رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: Mwanamke wa kabila la Juhaynah (Al-Ghamidiya) alienda kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akiwa na mimba ya zinaa, akamuambia: “Ee Nabiy wa Allaah! Nimestahiki haddi (adhabu) kwa hivyo nisimamishie.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuita msimamizi wake akamuambia: “Mfanyie wema, atakapojifungua[9] mlete.” Akafanya hivyo akaja naye, akaamuru, akafungwa kwa nguo zake kisha akaamuru akarajumiwa kisha akamswalia. ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) akamuambia: “Ee Nabiy wa Allaah! Unamswalia na hali amezini?” Akasema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) : “Kwa yakini ametubia tawbah ambayo lau ingaligawanyiwa kwa watu sabini mongoni mwa watu wa Madiynah, ingaliwatosha. Je ushawahi kuona lililo bora kuliko yeye kujileta mwenyewe kwa Allaah?” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1041.

وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {رَجَمَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏رَجُلًا مَنْ أَسْلَمَ، وَرَجُلًا مِنْ اَلْيَهُودِ، وَاِمْرَأَةً} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَقِصَّةُ رَجْمِ اَلْيَهُودِيَّيْنِ فِي "اَلصَّحِيحَيْنِ" مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عُمَرَ

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimpiga mawe (Rajm) mtu wa kabila la Aslam, na mtu mwigine wa Kiyahudi na mwanamke.[10] [Imetolewa na Muslim]

Kisa cha Mayahudi wawili kiko katika Swahiyh mbili; Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim  kutoka katika Hadiyth ya ‘Ibn Umar

 

 

 

1042.

وَعَنْ سَعِيدِ بْنِ سَعْدِ بْنِ عِبَادَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَ بَيْنَ أَبْيَاتِنَا رُوَيْجِلٌ ضَعِيفٌ، فَخَبَثَ بِأَمَةٍ مِنْ إِمَائِهِمْ، فَذَكَرَ ذَلِكَ سَعْدٌ لِرَسُولِ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏فَقَالَ: "اِضْرِبُوهُ حَدَّهُ".‏ فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنَّهُ أَضْعَفُ مِنْ ذَلِكَ، فَقَالَ: "خُذُوا عِثْكَالًا فِيهِ مِائَةُ شِمْرَاخٍ، ثُمَّ اِضْرِبُوهُ بِهِ ضَرْبَةً وَاحِدَةً".‏ فَفَعَلُوا} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَإِسْنَادُهُ حَسَنٌ .‏ لَكِنْ اخْتُلِفَ فِي وَصْلِهِ وَإِرْسَالِهِ

Kutoka kwa Sa’iyd bin Sa’d bin ‘Ubaadah[11] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Katika nyumba zetu kulikuwa na mtu dhaifu akazini na kijakazi miongoni mwa vijakazi vyao. Sa’d akamueleza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) khabari hiyo, akasema Rasuli wa Allaah: “Mmpigeni haddi (adhabu) yake.”[12] Maswahaba wakamuambia: “Ee Rasuli wa Allaah! Yeye ni dhaifu mno kuliko hiyo (haddi).” Rasuli akasema: “Chukueni shina la mtende lenye vitawi mia na mumpige nalo mara moja.” Maswahaba wakafanya hivyo. [Imetolewa na Ahmad, An-Nasaaiy na Ibn Maajah. Sanad ya wapokezi wake ni Hasan. Hata hivyo wametofautiana kama ni mawsuwl au mursal]

 

 

 

1043.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏قَالَ: {مَنْ وَجَدْتُمُوهُ يَعْمَلُ عَمَلَ قَوْمِ لُوطٍ، فَاقْتُلُوا اَلْفَاعِلَ وَالْمَفْعُولَ بِهِ، وَمَنْ وَجَدْتُمُوهُ وَقَعَ عَلَى بَهِيمَةٍ، فَاقْتُلُوهُ وَاقْتُلُوا اَلْبَهِيمَةَ}‏ رَوَاهُ أَحْمَدُ وَالْأَرْبَعَةُ،‏ وَرِجَالُهُ مُوَثَّقُونَ، إِلَّا أَنَّ فِيهِ اِخْتِلَافًا

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mtakayemkuta akifanya kitendo cha uliwati muuweni mwenye kufanya na kufanyiwa,[13] na mtu akimkuta akimuingilia mnyama basi muuweni yeye na muuweni mnyama.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah). Wapokezi wake ni madhubuti lakini ndani yake kuna ikhtilafu]

 

 

 

1044.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا: {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏ضَرَبَ وَغَرَّبَ وَأَنَّ أَبَا بَكْرٍ ضَرَبَ وَغَرَّبَ} رَوَاهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ، إِلَّا أَنَّهُ اخْتُلِفَ فِي رَفْعِهِ، وَوَقْفِهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alichapa mijeledi na akawatoa[14] mjini. Abuu Bakr alichapa na akatoa mjini. [Imetolewa na At-Tirmidhiy na wapokezi wake ni madhubuti, isipokuwa wamekhitilafiana kuwa ni mawquwf au Marfuw’]

 

 

 

1045.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: لَعَنَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏اَلْمُخَنَّثِينَ مِنْ اَلرِّجَالِ، وَالْمُتَرَجِّلَاتِ مِنْ اَلنِّسَاءِ، وَقَالَ: {أَخْرِجُوهُمْ مِنْ بُيُوتِكُمْ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume.[15] Na akasema: “Watoeni majumbani mwenu.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1046.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{اِدْفَعُوا اَلْحُدُودَ، مَا وَجَدْتُمْ لَهَا مَدْفَعًا} أَخْرَجَهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَإِسْنَادُهُ ضَعِيفٌ

وَأَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَالْحَاكِمُ: مِنْ حَدِيثِ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا بِلَفْظِ {ادْرَأُوا اَلْحُدُودَ عَنْ اَلْمُسْلِمِينَ مَا اِسْتَطَعْتُمْ} " وَهُوَ ضَعِيفٌ أَيْضًا

وَرَوَاهُ اَلْبَيْهَقِيُّ: عَنْ عَلِيٍّ ‏ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ ‏ (مِنْ)‏ قَوْلِهِ بِلَفْظِ:{ادْرَأُوا اَلْحُدُودَ بِالشُّبُهَاتِ}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Zuieni adhabu mnapopata njia ya kuzizuia.” [Imetolewa na Ibn Maajah kwa isnaad dhaifu]

Na At-Tirmidhiy amepokea na Al-Haakim kutoka katika Hadiyth ya ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) kwa tamshi: “Waepushieni adhabu[16] Waislam kadiri muwezavyo.” [nayo pia ni dhaifu]

Al-Bayhaqiyy amepokea kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwa kauli yake: “Epusheni haddi (adhabu) kwa shubha (utata).”

 

 

 

1047.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ ‏{اِجْتَنِبُوا هَذِهِ اَلْقَاذُورَاتِ اَلَّتِي نَهَى اَللَّهُ تَعَالَى عَنْهَا، فَمَنْ أَلَمَّ بِهَا فَلْيَسْتَتِرْ بِسِتْرِ اَللَّهِ تَعَالَى، وَلِيَتُبْ إِلَى اَللَّهِ تَعَالَى، فَإِنَّهُ مَنْ يَبْدِ لَنَا صَفْحَتَهُ نُقِمْ عَلَيْهِ كِتَابَ اَللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ} رَوَاهُ اَلْحَاكِمُ، وَهُوَ فِي "اَلْمُوْطَّإِ" مِنْ مَرَاسِيلِ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Jiepusheni na machafu haya Aliyokataza Allaah. Atakayetenda basi ajisitiri kwa sitara ya Allaah na atubu kwa Allaah, kwani atakayetudhihirishia hakika yake tutamsimamishia Kitabu Cha Allaah.” [Imetolewa na Al-Haakim, hadiyth hii iko katika kitabu cha Al-Muwatwa ya Imaam Malik kutoka katika Ahaadiyth za Zayd bin Aslama[17]]

 

[1] Huduwd ni wingi wa Hadd, ambayo ina maana ya ‘Kuzuia’. Ni adhabu ya kishariy’ah kwa wazinifu na mfano wa adhabu hizo huitwa kuwa ni Huduwd kwani zinaonesha adhabu kwa aina za watu waliotajwa. Wakati mwingine neno Hadd hutumika kutaja aina fulani  ya tendo la dhambi.

[2] Hadiyth hii inaonesha hukumu ya mtu aliyezini kwa Bikra awe ni mwanamme au mwanamke ni mijeledi mia moja na kuhamishwa kwenye nje ya dola ya Kiislam kwa muda wa mwaka mmoja. Kupigwa mijeledi mia moja ni kutokana na hukumu ya Qur-aan wakati adhabu kuhamishwa ni ziada inayokubaliwa na wapokezi wote wa Hadiyth. Adhabu ya mzinifu aliyekuishaoa au kuolewa ni Rajm (adhabu ya kupigwa mawe mpaka kufa) hadi kufa kulingana na makubaliano ya ‘Ulamaa. Hii inathibitisha vile vile kuwa kukiri kwa mmoja katika wazinifu kunatosha kusimamisha adhabu.

[3] Hii inakusudia maelezo ya Allaah katika Suwrah Al-Maaidah (5) Aayah 15:

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾

 

“Enyi Ahlal-Kitaab! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na anasamehe mengi. Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainisha”

 

[4] Hadiyth hii inamaanisha kuwa mzinifu wa kike na mzinifu wa kiume watapigwa mijeledi kisha wapigwe mawe (Rajm) hadi kufa. Hata hivyo, maoni ya ‘Ulamaa wengi ni kuwa suala la kupigwa mijeledi mia moja halina haja bali Rajm itatosheleza. Wamesema kuwa suala hili halina nguvu kwa sababu Nabiy hakumpiga Maa’iz na wengine, bali ni kupigwa mawe tu.

[5] Mtu ambaye alitoa uthibitisho huu alikuwa ni Maa’iz Aslami. Hadiyth hii inaelezea kuwa Qadhi ni lazima afanye uchunguzi wa kutosha kabla ya kutoa hukumu yake kuhusu adhabu fulani, kwani huenda maisha ya mtu yakakatishwa kwa hukumu yenye makossa.

[6] Maa’iz ndiye aliyekiri kufanya kosa hili wakati akiwa na mke.

[7] Hadiyth hii imetajwa na Muhadithina wote isipokuwa An-Nasaai, kadhalika imepokewa na Maswahaba wengi wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Iliripotiwa na Ubay bin Ka’ab kuwa Suwrah Ahzaab ilikaribiana na Suwrah Baqarah. Nyingi katika Aayah za Suwrah hizo zilifanywa Nasikh au zilikuwa Mansuwkh. Ubay bin Ka’ab anahadithia: “Tulikuwa tunasoma Aayah hizi katika Suwrah hii hadi tunapofikia katika Aayah:

 

 ‘Pindi mwanamme aliyeowa na mwanamke aliyeolewa wanapozini warujumuni’ baadae, usomaji wa Aayah hii ukafutwa lakini hukumu yake ikabaki pale pale, ambayo vile vile ni aina ya naskh.

 

Hukumu ya uzinifu unahitaji ushahidi ufuatao: (a) mashahidi wane, (b) kukiri kwa mhusika, na (c) mimba. Sharti hili la tatu linawahusu wanawake tu, lakini Imaam Shaafi’iy na Imaam Abuu Haniyfah hawakubaliani nalo. Kwa wanaolikubali kama ni ushahidi, mwanamke ambaye hakuolewa (asiyekuwa mtumwa) ataadhibiwa ikiwa mimba yake itakuwa wazi.

[8] Suala la mamlaka ya mtumwa mwanamke au mwanamme limeachwa kwa anayemmiliki. Watu wote walobakia wanahukumiwa na Dola. Ikiwa mtumwa mwanamme alikuwa ameshaoa, hapa kutakuwa na rai tofauti miongoni mwa ‘Ulamaa ya kuwa mamlaka ya kumpa adhabu yatakuwa kwenye Dola au kwa mwenyewe mwenye kummiliki. Ama kijakazi akizini basi atachapwa mijeledi na adhabu ya kumpiga mawe haitotekelezwa kwake. Hata kupigwa kwake mijeledi haitozidi hamsini. Ushahidi wa hili ni Aayah katika Qur-aan inayosema:

فَإِذَا أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَاحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى الْمُحْصَنَاتِ مِنَ الْعَذَابِ  

 Na watakapohifadhiwa katika ndoa, kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu ya waliyowekewa wanawake walio huru (wasioolewa).

[An-Nisaa: 4: 25]

[9] Hadiyth hii inabainisha kuwa suala la adhabu la uzinifu halitakiwi kufanyika mapema kwa mwanamke ili iangaliwe kwanza kama ana mimba. Ikiwa kama ana mimba anatakiwa asubiriwe hadi atakapojifungua. Pindi mwanamke atakapojifungua, mwanamke anaweza kupewa adhabu kwa sharti kuwa suala la kumnyonyesha mtoto na kumlea limekadhibiwa mwanamke mwingine. Ikiwa mwanamke huyo hajapatikana suala la adhabu litaakhirishwa hadi mtoto atakapoachishwa ziwa. Hata kama mwanamke huyo hakuwahi kuolewa adhabu itaakhirishwa mpaka atakapojifungua. Katika hali hiyo inatakiwa atendewe wema na jamaa zake na si vizuri kumshutumu na kumtukana ambapo Shariy’ah hairuhusu.

[10] Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliwahukumu watu wane kupigwa Rajm katika wakati wake. Wa kwanza ni lile tukio la mwanamke, wa pili alikuwa mtu wa kabila la Banu Aslam (Maa’iz bin Maalik) na Mayahudi wawili (mwanamke na mwanamme). Hili linamaanisha kuwa hukumu za Shariy’ah zinahusika pia kwa makafiri kama zinavyotekelezwa kwa Waislam.

 

[11] Sa’iyd bin Sa’d bin ‘Ubaadah Al Answaar As-Sa’iyd alikuwa ni Swahaba. Inasemekana kwa wengine alikuwa ni Taabi’i, alikuwa ni madhubuti aliyepokea baadhi za Ahaadiyth. Alikuwa gavana wa Yemen wakati wa Ukhalifa wa ‘Aliy bin Abi Twaalib.

 

[12] Hadiyth hii inaelezea ikiwa mtu ambaye hajaoa akazini, lakini kulingana na hali yake ya udhaifu au maradhi, na pindi itakaposimamishwa adhabu kwake anaweza kufa kama atapigwa mijeledi mia moja, inatakiwa upole katika kutekeleza adhabu yenyewe. Idadi ya mijeledi mia moja haitopunguzwa, bali huenda fimbo ya kupigia ikawa ni ndogo zaidi. Hata hivyo kunaweza kuwa na tofauti ya kupiga na isiwe kwa nguvu zaidi kama katika hali ya kawaida.

[13] Kuna rai tofauti kwa ‘Ulamaa kuhusu adhabu ya liwati kwa mwanamme kumfanyia mwanamke, pamoja na kuwa hakuna Hadiyth maalum inayoainisha hilo zaidi ya adhabu ya kifo. Hii ina maana tofauti iliyopo ni jinsi ya kutekeleza adhabu yenyewe tu. Baadhi wanaona kuwa adhabu ni Rajm (kupigwa kwa mawe). Wengine wanaona kuwa watupwe kutoka umbali wa juu na kurushwa chini. Kundi lingine linaona kuwa wawashiwe moto. Rai nyingine inaona kuwa hukumu ya mzinifu ipite kwake; Kama ameoa arajimiwe; vinginevyo, apigwe mijeledi mia moja na atolewe nje ya mji. Allaah ndiye Mjuzi.

 

[14] Baadhi ya ‘Ulamaa wana muono kuwa adhabu ya kuhamishwa mji imefutwa na haifanyi kazi tena. Hadiyth hii inapinga ile rai ya kuwa ikiwa wazinifu walihamishwa miji wakati wa Makhalifa waongofu, dalili ipi inayoonesha kuwa hukumu hii imefutwa?

 

[15] Hadiyth hii inathibitisha kuwa mwanamke au mwanamme ambaye anaiga tabia ya jinsia ya pili ni watu wenye kulaaniwa na jambo hili ni katika madhambi. Matowashi wapo wa aina mbili: ni wale matowashi ambao maumbile yao ya kiwiliwili yanafanana na wanawake na wakati wengine wanafanana na wanaume. Matowashi lazima wavae nguo zinazofanana na jinsia yao na kufanana nao zaidi.

[16] Ikiwa kuna shaka kuhusu ukweli fulani wa ushahidi unaopelekea katika hukumu ya adhabu, hukumu ile inabidi itenguliwe. Hadiyth hii haikusudii kuwa hakuna hukumu itakayotolewa, bali inamaanisha kuwa hukumu ya adhabu haitopitishwa hadi tatizo liwe la wazi uwazi usio na shaka. Watu wanashauriwa kuwa wasipeleke kesi yoyote mahakamani hadi wajenge ushahidi wa kutosha unaowaunga katika madai yao ili kuthibitisha kuwa fulani ni mwenye kosa.

[17] Alikuwa ni Swahaba kutoka kabila la Al-Balawi. Alikuwa katika ukoo wa Banuu Al-‘Ajlan, washirika wa Banuu ‘Amr bin ‘Awf katika Al-Answaar. Alishuhudia Badr na kadhalika Swiffiyn akiwa pamoja na ‘Aliy. Hata hivyo, Hishaam Al-Kalabi amesema, (Zaid) aliuwawa na Twulayha bin Khuwaylid Al-Asad katika siku ya Bazakha katika mwaka wa 11 Hijriyyah mwanzoni mwa Ukhalifa wa Abuu Bakr.

Share