12-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwenye Hedhi Au Nifaas Akitoharika Alasiri Je Anawajibika Kuswali Swalaah Ya Adhuhuri Na Alasiri?

 

12-Mwenye Hedhi Au Nifaas Akitoharika Alasiri

Je Anawajibika Kuswali Swalaah Ya Adhuhuri Na Alasiri?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Akitoharika mwenye hedhi na nifasi wakati wa Alasiri je, itamlazimu kuswali Swalaah ya Adhuhurii na Alasiri au ataswali Adhuhuri tu?

 

 

JIBU:

 

 

Kauli iliyokubaliwa zaidi katika masuala haya itampasa aswali Alasiri tu. Kwani hakuna dalili ya kupasa kuswali Adhuhuri na asili yake ni 'Baraatu Dhimma' kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayediriki rakaa moja ya Alasiri kabla ya kuzama jua atakuwa amediriki Alasiri.” wala hakutaja kudiriki Adhuhuri na kama Adhuhuri ingekuwa ni wajibu basi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  angebainisha.

 

Na lau mwanamke angeanza hedhi yake baada ya kuingia Adhuhuri haitomlazimu isipokuwa kulipa Swalaah ya Adhuhuri bila ya Alasiri pamoja ya kuwa Adhuhuri inakusanywa pamoja na Alasiri.

 

Hii haitofautiani na hali ya swali la awali. Hivyo kauli inayochukuliwa ni kuwa haimlazimu isipokuwa Swalaah ya Alasiri pekee kwa dalili ya andiko na qiyaas juu yake.

 

Vivyo hivyo hali lau akitoharika kabla ya kutoka wakati wa ‘Ishaa basi haimlazimu isipokuwa Swalaah ya ‘Ishaa wala halazimikii Swalaah ya Magharibi.

 

Share