13-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mimba Ikitoka Kabla Ya Kuumbika Kichanga Na Baada Ya Kuumbika Nini Hukmu Ya Swawm?

 

13-Mimba Ikitoka Kabla Ya Kuumbika Kichanga Na Baada Ya Kuumbika

Nini Hukmu Ya Swawm?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Baadhi ya wanawake waliotoa mimba hali yao ni kama hivyo: Ima mimba iwe imetoka kabla ya kuumbwa kichanga au imetoka baada ya kuumbwa kwake. Ni nini hukumu ya Swawm yake katika siku ile iliyotoka mimba na Swawm ya masiku ambayo ameona damu?

 

 

JIBU:

 

 

Ikiwa kichanga bado hakijaumbwa basi damu yake hii sio damu ya nifaas, na hivyo anawajibika Swawm na Swalaah na Swawm yake itakuwa ni sahihi.  Na ikiwa kichanga kimeumbika basi damu hiyo ni damu ya nifaas  na haimpasi kuswali wala Swawm. 

 

 

Na Shariy’ah katika mas-ala haya ni kwamba  ikiwa  kichanga kimeshaumbwa basi ni damu ya nifaas, na ikiwa hakijaumbwa basi sio damu ya nifaas, na ikiwa ni damu ya nifaas basi inakuwa kwake haraam kile kilichoharamishwa kwa wenye nifaas na ikiwa sio damu ya nifaas, basi sio haraam kwake hilo.

 

 

Share