Pilau Ya Nyama Na Mtindi

Pilau Ya Nyama Na Mtindi

 

VIPIMO

Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili(LB)

Mchele Basmati - 2 Magi

Chumvi ya wali - kiasi

Kitungu kilichokatwa katwa - 1 kikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu  

Mtindi (yogurt) - ½ kikombe

Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari - 2 vijiko vya supu 

Mafuta kidogo yakukaangia

Rangi ya manjano (ukipenda)

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

 Osha mchele na roweka nusu saa .

 Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).

Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.

Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga hadi nyama isiwe nyekundu tena.

Tia maji gilasi 1½- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.

Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.

Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.

Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.

Changanya  wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.

 

 

Share