24-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Baada Ya Miezi Miwili Ya Nifaas Akatoharika Ameona Matone Ya Damu Aache Swalaah Na Swiyaam

 

 Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

24-Baada Ya Miezi Miwili Ya Nifaas  Akatoharika

Ameona  Matone Ya Damu Aache Swalaah Na Swiyaam

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Anauliza muulizaji: Mwanamke baada ya miezi miwili ya Nifaas na baada ya kutoharika anaona matone madogo ya damu je atafungua na haswali? Au afanye nini?

 

 

JIBU:

 

Matatizo ya mwanamke kuhusu hedhi na nifaas  ni bahari isiyo na pwani.  Sababu mojawapo ni kutumia vidonge hivi vyenye kuzuia mimba na vyenye kuzuia hedhi na watu wengi hawayajui matatizo haya makubwa. Ni kweli matatizo haya yapo tokea kwa kutimilizwa Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  bali tokea kuwepo kwa mwanamke ulimwenguni,  isipokuwa uwepo wake unaomfanya mtu kutatizika unaowapata watu wengi katika kufikia suluhisho lake ni jambo la kusikitisha sana.

 

 

Hata hivyo kawaida ya Shariy’ah ni kuwa mwanamke akitoharika na akiona tohara anayoiamini na yakini katika hedhi na nifaas; nakusudia tohara ya hedhi kutoka kwa maji meupe yanayojulikana na wanawake je baada ya tohara kuna maji machafu au manjano au umajimaji; zote hizi sio hedhi, hivyo haimzuii na Swalaah wala Swiyaam, wala jimai ya mtu kwa mke wake kwa sababu sio hedhi. Ummu ‘Atwiyyah amesema, ‘Tulikuwa hatuoni umanjano na umajimaji kuwa ni kitu’ [Al-Bukhari] na Abuu Daawuwd akazidisha: “Baada ya tohara.” Na Isnaad yake ni Swahiyh.

 

 

Kwa haya tunasema: Kila kinachotokea baada ya tohara yakini kwa mambo haya haimdhuru mwanamke na haimzuii na Swalaah yake wala Swiyaam zake wala  kuingiliwa na mumewe, bali yapasa tusifanye haraka hadi tuone tohara, kwa sababu baadhi ya wanawake damu ikikauka anafanya haraka kukoga kabla ya kuona tohara. Hili liliwafanya wanawake Maswahaba wakienda kwa mama wa waumini ‘Aaishah  (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa) wakienda na pamba ikiwa na damu na ‘Aiashah akiwaambia: “Msifanye haraka hadi muone maji meupe.”.

 

 

Share