32-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Amepata Hedhi Wakati Anaswali Afanyeje Na Je Alipe Swalaah Muda Wa Hedhi?

 

 Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

31-Amepata Hedhi Wakati Anaswali Afanyeje

Na Je Alipe Swalaah Muda Wa Hedhi?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Niliingia katika ada ya mwezi (hedhi) wakati wa Swalaah, Je, nifanye nini? Je nilipe Swalaah katika muda wote wa ada yangu

 

 

JIBU:

 

Ikitokezea umeingia katika hedhi baada ya kuingia wakati wa Swalaah kwa mfano kuingia mwezini baada ya kuzama (zawaal) kwa nusa saa, basi yeye baada ya kutoharika na hedhi atailipa Swalaah hii ambao umeingia wakati wake naye akiwa mwenye tohara kwa kauli yake  Ta’aalaa:

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا 

Hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu. [An-Nisaa (4:103)]

 

Wala hatolipa Swalaah wakati wa hedhi kwa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ndefu:

أليست إذا حاضت لم تصل ولم تصم

“Je si akiwa mwezini haswali na hafungi…”  

 

‘Ulamaa wamekubaliana kuwa mwanamke halipi Swalaah iliyompita alipokuwa wakati wa hedhi. Ama akitoharika na ikabakia wakati kiasi cha rakaa moja na zaidi ya hapo basi huswali wakati ule aliotoharika kwa kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Atakayediriki rakaa katika Swalaah ya Alasiri kabla ya kuzama kwa jua basi huyu amediriki Swalaah ya Alasiri.”

 

Akitoharika wakati wa Alasiri au kabla ya kuchomoza kwa jua na akawa amebaki hadi kuzama kwa jua au kuchomoza kwake kiasi cha rakaa moja basi ataswali Alasiri katika masuala ya mwanzo na Alfajiri katika masuala ya pili.

 

Share