37-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Mwanamke Anayetokwa Majimaji Je, Inajuzu Aswali Swalaah Ya Adhw-Dhwuhaa Kwa Wudhuu Wa Alfajiri?

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

37-Mwanamke Anayetokwa Majimaji

Je, Inajuzu Aswali Swalaah Ya Adhw-Dhwuhaa Kwa Wudhuu Wa Alfajiri?  

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Je, ni sahihi mwanamke  (anayetokwa majimaji)

kuswali  Swalaah ya Adhw-Dhwuhaa  kwa  udhuu  wa  (Swalaah ya) Alfajiri?

 

 

 

JIBU:

 

 

Haisihi kwa kuwa Swalaah ya Adhw-Dhwuhaa  imewekwa muda  maalum hivyo basi hapana budi kuchukuwa  wudhuu  unapoingia  wakati  wake kwa sababu mwanamke huyu ni kama vile mustahaadhah, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  ameamrisha  Mustahadhah achukue udhu katika kila Swalaah.

 

 Wakati wa Adhuhuri ni: Pindi  jua linapokuwa katikatika hadi wakati wa Alasiri.

 

Wakati  wa Alasiri ni:  Kutoka kwa wakati wa Adhuhuri hadi jua linapokuwa  la njano au mpaka linapokaribia kuzama. Katika hali yake ya dharura ni kuzama kwa jua.

 

Wakati  wa Magharibi ni:  Kuzama kwa jua hadi kuondoka wekundu wa jua.

 

Wakati  wa ‘Ishaa ni: Kupotea wekudu wa jua hadi katikati ya usiku.

 

Share