46-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Yanayomtoka Kabla Ya Hedhi Kama Uzi Wa Rangi Nyeusi Au Buni

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

46-Yanayomtoka Kabla Ya Hedhi Kama Uzi Wa Rangi Nyeusi Au Buni  

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

 

Ni nini hukumu ya majimaji yale machafu (yanayoelekea kwenye wekundu au wanavyosema Fuqahaa maji yaliyochanganyika na udongo) yanayotoka kwa mwanamke kabla ya hedhi kwa siku au zaidi au chini ya hapo. Inaweza kuwa inateremka kwa njia ya uzi uzi mweusi au rangu ya buni mwembamba?

 

 

JIBU:

 

 

Hii ikiwa ni miongoni mwa vitangulizi vya hedhi basi hiyo ni sehemu ya hedhi na hilo huambatana na maumivu na tumbo kukatika katika na baada ya hapo ada yake inaanza. Ama yale majimaji machafu (yanayoelekea kwenye wekundu au wanavyosema Fuqahaa maji yaliyochanganyika na udongo) yanayotoka baada ya hedhi hiyo itasubiriwa hadi itakapoteremka; kwani majimaji hayo yaliyoambatana na hedhi ni hedhi kwa kauli ya  ‘Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa):

 

لا تعجلن حتى ترين القصة البيضاء

“Wala usifanye haraka hadi utakapoona majimaji meupe.”

 

Allaah Ndiye mjuzi zaidi

 

Share