47-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ihraam Haina Swalaah Na Hukmu Ya Mwenye Hedhi Kusoma Qur-aan

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

47-Ihraam Haina Swalaah Na Hukmu Ya Mwenye Hedhi Kusoma Qur-aan

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Mwenye hedhi ataswali vipi rakaa mbili za Ihraam? Na je yampasa mwanamke mwenye hedhi kusomasoma Aayah katika hali ya siri (moyoni)?

 

 

JIBU:

 

Kwanza kabisa yapasa kujua kuwa Ihraam haina Swalaah, hivyo haikupokewa kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amelazimisha kwa umma wake Swalaah ya Ihraam wala hakuonesha kwa matendo yake au kukiri.

 

Pili: Kuwa mwanamke huyu mwenye hedhi ambaye amekuwa na hedhi kabla ya kuhirimia anaweza kuhirimia akiwa ni mwenye hedhi kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alimuamrisha Asmaa bint ‘Umays  mke wa Abuu Bakar  alipokuwa na nifaas katika Dhul-Hulayfah ni kuwa akoge na azungushe nguo na ahirimie. Vivyo hivyo kwa mwenye hedhi na ataendelea kubaki kwenye ihraam yake hadi atoharike, kisha baada ya hapo atatufu na kufanya Sa’yi.

 

Ama kauli yake katika swali: Je yafaa kwake kusoma Qur-aan? Naam, mwenye hedhi ana haki kusoma Qur-aan  atakapokuwa na haja ya kufanya hivyo au maslahi fulani. Ama kama hakuna haja au maslahi fulani kusoma kwake kama ni kwa ajili ya kuabudu na kujikurubisha na Allaah ni bora asifanye hivyo.

 

Share