55-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ametoka Mji Mmoja Kukusudia ‘Umrah Mkewe Alikuwa Katika Hedhi Akakamilisha ‘Umrah Bila Mkewe

 

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

55-Ametoka Mji Mmoja Kukusudia ‘Umrah Mkewe Alikuwa Katika Hedhi  

Akakamilisha ‘Umrah Bila Mkewe

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Muulizaji anauliza: Nimetokea Yanbu’ kwenda kwenye ‘Umrah mimi pamoja na familia yangu lakini nilipofika Jeddah mke wangu akaingia kwenye ada yake ya mwezi ama mimi nilikamilisha ‘Umrah peke yangu bila ya mke wangu, ni ipi hukumu inayomhusu mke wangu?

 

 

JIBU:

 

 

Hukumu inayomhusu mke wako ni kuwa abakie hadi atoharike kisha alipe ‘Umrah yake, kwa sababu wakati Mama wa Waumini Swafiyyah alipopatwa na hedhi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alisema: “Yeye ametuzuia.” Wakasema kuwa Swafiyyah ameshafanya Twawaaf Al-Ifaadhwah. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:  “Basi ajifunge funge.” Hivyo basi kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  “Yeye ametuzuia.” Ni dalili ya kuwa ni waajbi kwa mwanamke kubaki akiwa na hedhi kabla ya kufanya Twawaaf Al-Ifaadhwah hadi atoharike kisha atufu na kadhalika Twawaaf ya ‘Umrah mfano wake ni Twawaaf Al-Ifaadhwah kwa sababu ni nguzo katika ‘Umrah. Hivyo basi akiwa na hedhi aliyekwenda kufanya ‘Umrah kabla ya Twawaaf atasubiri hadi atoharike kisha atatufu.

 

Share