030-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uombezi (shifaa)

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الشفاعة

030-Mlango Wa Uombezi (shifaa)

 

Alhidaaya.com

 

:قَالَ الله تَعَالَى

 

مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا ﴿٨٥﴾

Atakayeombea uombezi mzuri atapata fungu lake katika hayo. Na atakayeombea uombezi mbaya atapata sehemu yake katika hayo. Na Allaah daima ni Mwenye kudhibiti na Mwangalizi wa kila kitu. [An-Nisaa: 85]  

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه، قَالَ: كَانَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم إِذَا أتاهُ طَالِبُ حَاجَةٍ أقبَلَ عَلَى جُلَسَائِهِ ، فَقَالَ : (( اشْفَعُوا تُؤْجَرُوا ، وَيَقْضِي الله عَلَى لِسَانِ نَبِيِّهِ مَاأحبَّ)) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : (( مَا شَاءَ )) .

 

Na imepokewa kutoka kwake Abuu Muwsaa Al Ash'aariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anajiliwa na mwenye haja, huwaelekea walioketi naye akiwaambia: " Ombeni mtalipwa, na Allaah Hukidhi (haja) kwa ulimi wa Rasuli Wake Anavyopenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah nyingine: " Anavyotaka".

 

 

Hadiyth – 2

 

وعن ابن عباس رضي الله عنهما في قِصَّةِ برِيرَةَ وَزَوْجِهَا ، قَالَ : قَالَ لَهَا النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( لَوْ رَاجَعْتِهِ ؟ )) قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللهِ تَأمُرُنِي ؟ قَالَ : (( إنَّمَا    أَشْفَع )) قَالَتْ : لاَ حَاجَةَ لِي فِيهِ . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) Kuhusianana kisa cha Bariyrah na mumewe, Akasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Waonaje lau ungerudi kwake?" Akasema (Bariyrah): " Ee Rasuli wa Allaah! Unaniamuru?" Akamjibu: "Hakika mimi naombea." Akasema (Bariyrah): "Sina haja naye." [Al-Bukhaariy]

 

 

Share