044-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuwaheshimu Wanazuoni, Wakubwa na Watu Watukufu na Kuwatanguliza Juu ya Wengine, Kutukuza Vikao Vyao na Kudhihirisha Utukufu Wao

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب توقير العلماء والكبار وأهل الفضل وتقديمهم عَلَى غيرهم ورفع مجالسهم وإظهار مرتبتهم

044-Mlango Wa Kuwaheshimu Wanazuoni, Wakubwa na Watu Watukufu na Kuwatanguliza Juu ya Wengine, Kutukuza Vikao Vyao na Kudhihirisha Utukufu Wao

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾

Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu.[Az-Zumar: 9]

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي مسعودٍ عقبةَ بن عمرو البدري الأنصاري رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَؤُمُّ القَوْمَ أقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ الله ، فَإنْ كَانُوا في القِراءةِ سَوَاءً ، فأَعْلَمُهُمْ بِالسُّنَّةِ ، فَإنْ كَانُوا في السُّنَّةِ سَوَاءً ، فَأَقْدَمُهُمْ هِجْرَةً ، فَإنْ كَانُوا في الهِجْرَةِ سَوَاءً ، فَأقْدَمُهُمْ سِنّاً ، وَلاَ يُؤمّنَّ الرَّجُلُ الرَّجُلَ في سُلْطَانِهِ ، وَلاَ يَقْعُدْ في بَيْتِهِ عَلَى تَكْرِمَتِهِ إلاَّ بِإذْنهِ )) رواه مسلم .

وفي رواية لَهُ : (( فَأقْدَمُهُمْ سِلْماً )) بَدَلَ (( سِنّاً )) : أيْ إسْلاماً . وفي رواية :  (( يَؤُمُّ القَومَ أقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ اللهِ ، وَأقْدَمُهُمْ قِراءةً ، فَإنْ كَانَتْ قِرَاءتُهُمْ سَوَاءً فَيَؤُمُّهُمْ أقْدَمُهُمْ هِجْرَةً ، فَإنْ كَانُوا في الهِجْرَةِ سَواء ، فَليَؤُمُّهُمْ أكْبَرُهُمْ سِنّاً )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uud 'Uqbah bin 'Amru Al-Badriy Al-Answaarriyy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aswalishe msomi wao wa Kitabu cha Allaah. Ikiwa wako sawa katika kisomo, basi mjuzi zaidi katika Sunnah. Ikiwa wako sawa katika Sunnah, wa mwanzo wao kuhama. Wakiwa sawa katika kuhama, basi mkubwa wao wa umri, Wala mtu hamswalishi mwingine katika mamlaka yake ila kwa idhini yake, wala asikae katika utukufu wake ila kwa ruhusa yake." [Muslim]

Katika riwaayah yake: "Wa mwanzo kusilimu" badala ya "umri mkubwa." 

Katika riwaayah nyengine: "Aswalisha watu msomi wao kwa Kitabu cha Allaah , na wa mwanzo wao kusoma,. Ikiwa kisomo chao ni sawa, basi aswalishe wa mwanzo wao kuhama. Ikiwa wapo sawa katika kuhama, basi mkubwa wao."

  

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي مسعودٍ عقبةَ بن عمرو البدري الأنصاري رضي الله عنه، قَالَ : كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَمْسَحُ مَنَاكِبَنَا في الصَّلاةِ ، ويَقُولُ : (( اسْتَوُوا وَلاَ تَخْتَلِفُوا ، فَتَخْتَلِفَ قُلُوبُكُمْ ، لِيَلِني مِنْكُمْ أُولُوا الأحْلاَمِ وَالنُّهَى ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uud 'Uqbah bin 'Amru Al-Badriy Al-Answaarriyy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akifuta mabega yetu katika swalaah na kusema: "Nyookeni wala msikhitilafiane zikatofautiana nyoyo zenu. Wanikaribie wenye utambuzi na akili miongoni mwenu, kisha wanaowafuatia wao, kisha wanaowafuatia wao." [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لِيَلِني مِنْكُمْ أُولُوا الأحْلام وَالنُّهَى ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ )) ثَلاثاً (( وَإيَّاكُمْ وَهَيْشَاتِ الأسْوَاق )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wanikaribie wenye akili na utambuzi miongoni mwenu, kisha wanaowafuatia wao (mara tatu) na nawatahadharisheni sana na vurumai na tangamano la watu wa masokoni." [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي يَحيَى ، وقيل : أَبي محمد سهلِ بن أَبي حَثْمة - بفتح الحاءِ المهملة وإسكان الثاءِ المثلثةِ - الأنصاري رضي الله عنه، قَالَ : انطَلَقَ عَبدُ اللهِ بنُ سهْلٍ وَمُحَيِّصَة بن مَسْعُود إِلَى خَيْبَرَ وَهِيَ يَومَئذٍ صُلْحٌ ، فَتَفَرَّقَا ، فَأتَى مُحَيِّصَةُ إِلَى عبدِ اللهِ ابنِ سهل وَهُوَ يَتشَحَّطُ في دَمِهِ قَتِيلاً ، فَدَفَنَهُ ، ثُمَّ قَدِمَ المَدِينَةَ فَانْطَلَقَ عَبدُ الرحمان ابنُ سهل وَمُحَيِّصَةُ وحوَيِّصَةُ ابْنَا مَسْعُودٍ إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَذَهَبَ عَبدُ الرحمان يَتَكَلَّمُ ، فَقَالَ : (( كَبِّرْ كَبِّرْ )) وَهُوَ أحْدَثُ القَوم ، فَسَكَتَ ، فَتَكَلَّمَا ، فَقَالَ : (( أتَحْلِفُونَ وتَسْتَحِقُّونَ قَاتِلَكُمْ ؟ … )) وذكر تمام الحديث . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Amesema Abu Yahyaa au Abu Muhammad Sahl bin Abi Hathmah: 'Abdillaahi bin Sahl, Muhayyiswah bin Mas'uud waliekea Khaybar wakati wa sulhu. Wakaachana. Muhayyiswah akamjia 'Abdillaahi bin Sahl akiwa ameolewa damu ameuwawa, Akamzika akarudi Madiynah. Wakaenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), 'Abdur-Rahman bin Sahl, Muhayyiswah na Huwayyiswah watoto wa Mas'uud. 'Abdur-Rahman akazungumza. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Azungumze mkubwa wenu" Nae alikuwa mdogo wao, akanyamaza. Wakazungumza wawili wao. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, mtaapa ili mstahiki fidia kwa muuaji wenu?" Akataja ukamilifu wa Hadiyth. [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

 

 

Hadiyth – 5

وعن جابر رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَجْمَعُ بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ مِنْ قَتْلَى أُحُد يَعْنِي في القَبْرِ ، ثُمَّ يَقُولُ : (( أيُّهُما أكْثَرُ أخذاً للقُرآنِ ؟ )) فَإذَا أُشيرَ لَهُ إِلَى أحَدِهِمَا قَدَّمَهُ في اللَّحْدِ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijumuisha watu wawili katika waliouliwa Uhud, yaani katika kaburi; kisha hutuuliza: "Ni yupi kati yao amehifadhi Qur-aan?" Anapoashiriwa mmoja wao anamtanguliza katika mwana ndani." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Hadiyth – 6

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( أرَانِي فِي المَنَامِ أتَسَوَّكُ بِسِوَاكٍ ، فَجَاءنِي رَجُلانِ ، أحَدُهُما أكبر مِنَ الآخرِ ، فَنَاوَلْتُ السِّوَاكَ الأصْغَرَ ، فَقِيلَ لِي : كَبِّرْ ، فَدَفَعْتهُ إِلَى الأكْبَرِ مِنْهُمَا )) رواه مسلم مسنداً والبخاري تعليقاً .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilijiona usingizini nikipiga msuwaki. Wakanijia watu wawili, mmoja wao ni mkubwa kuliko mwenziwe. Nikataka kumpa msuwaki yule mdogo, hapo nikaambiwa: "Mtangulize mkubwa". Nikampatia huyo mkubwa." [Muslim na Al-Bukhaariy]

 

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي موسى رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ مِنْ إجْلالِ اللهِ تَعَالَى : إكْرَامَ ذِي الشَّيْبَةِ المُسْلِمِ ، وَحَامِلِ القُرآنِ غَيْرِ الغَالِي فِيهِ ، وَالجَافِي عَنْهُ ، وَإكْرَامَ ذِي السُّلْطَانِ المُقْسِط )) حديث حسن رواه أَبُو داود .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muusa kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika katika Kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) ni kumkirimu mzee Muislamu, na kuiacha mbali bila kuitumia, na kumkirimu kiongozi muadilifu".  Hadiyth Hassan. [Abu Daawuud]

 

 

 

Hadiyth – 8

وعن عمرو بن شعيب ، عن أبيه ، عن جده  رضي الله عنهم، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَيْسَ مِنَّا مَنْ لَمْ يَرْحَمْ صَغِيرنَا ، وَيَعْرِفْ شَرَفَ كَبيرِنَا )) حديث صحيح رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

وفي رواية أبي داود : (( حَقَّ كَبيرِنَا )) .

Na imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Shu'ayb kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake (Radhwiyah Allaahu 'anhuma) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si katika sisi asiye warehemu wadogo wetu na kutambua heshima (utukufu) wa wakubwa wetu." Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Abu-Daawuud na At-Tirmidhiy, ambaye amesema: Hadiyth Hassan Swahiyh.

 

 

 

Hadiyth – 9

وعن ميمون بن أَبي شَبيب رحمه الله : أنَّ عائشة رَضي الله عنها مَرَّ بِهَا سَائِلٌ ، فَأعْطَتْهُ كِسْرَةً ، وَمَرَّ بِهَا رَجُلٌ عَلَيهِ ثِيَابٌ وَهَيْئَةٌ ، فَأقْعَدَتهُ ، فَأكَلَ ، فقِيلَ لَهَا في ذلِكَ ؟ فقَالتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أنْزِلُوا النَّاسَ مَنَازِلَهُمْ )) رواه أبو داود . لكن قال : ميمون لم يدرك عائشة . وقد ذكره مسلم في أول صحيحه تعليقاً فقال : وذكر عن عائشة رضي الله عنها قالت : أمرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم أن ننـزل الناس منازلهم ، وَذَكَرَهُ الحَاكِمُ أَبُو عبد الله في كتابه (( مَعرِفَة عُلُومِ الحَديث )) وَقالَ : (( هُوَ حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwake 'Maymuuna bin Abu Shabiyb (Rahimmahu Allaah) kuwa 'Aa'ishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) alipitiwa na mwombaji, naye akampatia kisra (mkate). Baadaye, akapita mtu aliyevaa vizuri, akamuomba, naye ('Aa'ishah) akamkalisha chini na akampatia chakula ili ale. Akaulizwa kuhusu hilo, naye akasema: "Rasuli wa Allaah amesema: Wawekeni watu katika vyeo vyao." [Abu Daawuud,aliyesema Maymuun hakukutana na 'Aa'ishah] Na imetajwa na Muslim mwanzo wa Sahihi yake, akasema: Na imetajwa kuwa 'Aa'ishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru kuweka watu katika vyeo vyao. Na Allaah ametuamuru kuwaweka watu kwa vyeo vyao." Ameitaja hiyo Al-Haakim Abu 'Abdillaahi katika kitabu chake (Ma'rifatu 'Uluumil Hadiyth) Akasema ni Hadiyth Swahiyh.

 

 

 

Hadiyth – 10

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَدِمَ عُيَيْنَةُ بنُ حِصْن ، فَنَزَلَ عَلَى ابْنِ أخِيهِ الحُرِّ بنِ قَيسٍ ، وَكَانَ مِنَ النَّفَرِ الَّذِينَ يُدْنِيهِمْ عُمرُ رضي الله عنه، وَكَانَ القُرَّاءُ أصْحَاب مَجْلِس عُمَرَ وَمُشاوَرَتِهِ ، كُهُولاً كاَنُوا أَوْ شُبَّاناً ، فَقَالَ عُيَيْنَةُ لابْنِ أخيهِ : يَا ابْنَ أخِي ، لَكَ وَجْهٌ عِنْدَ هَذَا الأمِيرِ ، فَاسْتَأذِنْ لِي عَلَيهِ ، فاسْتَأذَن له ، فَإذِنَ لَهُ عُمَرُ رضي الله عنه، فَلَمَّا دَخَلَ قَالَ : هِي يَا ابنَ الخَطَّابِ ، فَواللهِ مَا تُعْطِينَا الْجَزْلَ ، وَلا تَحْكُمُ فِينَا بالعَدْلِ ، فَغَضِبَ عُمَرُ رضي الله عنه حَتَّى هَمَّ أنْ يُوقِعَ بِهِ ، فَقَالَ لَهُ الحُرُّ : يَا أميرَ المُؤْمِنينَ ، إنَّ الله تَعَالَى قَالَ لِنَبيِّهِ صلى الله عليه وسلم: ( خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ) وَإنَّ هَذَا مِنَ الجَاهِلِينَ . واللهِ مَا جَاوَزَهاَ عُمَرُ حِينَ تَلاَهَا عليه ، وكَانَ وَقَّافاً عِنْدَ كِتَابِ اللهِ تَعَالَى . رواه البخاري .

Amesema Ibn 'Abbaas (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) Alikuja 'Uyaynah bin Hiswnakashukia kwa mtoto wa nduguye, Al-Hurr bin Qays, mtu wa karibu kwa 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwa ubora wake. Kamati ya shuura ya majlis ya 'Umar walikuwa wasomi, wazee na vijana. 'Uyaynah akamwambia mtoto wa nduguye: "Eemtoto wa ndugu yangu! Wewe una hadhi kwa huyu Amiri, niombee ruhusa nimuone." Akamuombea idhini, na 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akamruhusu Alipoingia alisema: "Hiy (kutishia), ee Ibn Al-Khatwtwaab: Wa-Allaahi hutupi zawadi wala hutuhukumu kwa uadilifu." Akakasirika 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akakaribia kumwadhibu, Al'Hurr akamwambia: "Ee Amiri wa Waumini! "Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aala) Alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili." [Al-A'raaf: 199] na huyu ni miongoni mwa wajinga." Wa-Allaahi, aliposikia maneno hayo alitulia tuli, kwani yeye ni mtu mwenye kufuata kabisa Kitabu cha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aala). [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي سعيد سَمُرة بنِ جُندب رضي الله عنه، قَالَ : لقد كنت عَلَى عَهْدِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم غُلاماً ، فَكُنْتُ أحْفَظُ عَنْهُ ، فَمَا يَمْنَعُنِي مِنَ القَوْلِ إلاَّ أنَّ هاهُنَا رِجَالاً هُمْ أسَنُّ مِنِّي . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

AmesemaAbu Sa'iyd Samurah bin Jundub (Radhwiyah Allaahu 'anhu): Hakika nilikuwa kijana katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nilikuwa ni mwenye kuhifadhi kutoka kwake. Hakunikataza mimi kuzungumza ila kulikuwepo na watu wakubwa (kiumri) kuniliko." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 12

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا أكْرَمَ شَابٌّ شَيْخاً لِسِنِّهِ إلاَّ قَيَّضَ الله لَهُ مَنْ يُكْرِمُهُ عِنْدَ سِنِّه )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث غريب )) .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hatomkirimu kijana mzee kwa ajili ya umri wake isipokuwa Allaah Atamtolea atakaye mkirimu katika uzee wake." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Ghariyb (ngeni)].

 

 

 

 

 

 

Share