00-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Vyakula

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

 

كِتَاب اَلْأَطْعِمَةِ

00-Kitabu Cha Vyakula

 

 

 

 

 

 

1134.

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه  عَنْ اَلنَّبِيِّ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {" كُلِّ ذِي نَابٍ مِنْ اَلسِّبَاعِ، فَأَكَلَهُ حَرَامٌ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

وَأَخْرَجَهُ: مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ عَبَّاسٍ بِلَفْظٍ: نَهَى.‏ وَزَادَ: {" وَكُلُّ ذِي مِخْلَبٍ مِنْ اَلطَّيْرِ"}

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila mnyama mwenye kuwinda kwa meno, kumla kwake ni haraam.”[1] [Imetolewa na Muslim]

Pia amepokea kutoka katika hadiyth ya ‘Abdullaah ibn ‘Abbaas kwa tamshi hili: “Amekataza.” Na akaongeza: “Na kila ndege anayewinda kwa kucha.”

 

 

 

1135.

وَعَنْ جَابِرٍ  رضى الله عنه  قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم يَوْمَ خَيْبَرَ عَنْ لُحُومِ اَلْحُمُرِ اَلْأَهْلِيَّةِ، وَأْذَنْ فِي لُحُومِ اَلْخَيْلِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.‏ ‏ وَفِي لَفْظِ اَلْبُخَارِيِّ: {وَرَخَّصَ}

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza nyama za punda kihongwe (wa mjini)[2] siku ya Vita vya Khaybar, akaruhusu nyama za farasi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

Na katika tamshi la Bukhaariy: “Na ameruhusu.”

 

 

 

1136.

وَعَنْ اِبْنِ أَبِي أَوْفَى قَالَ: {غَزَوْنَا مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم سَبْعَ غَزَوَاتٍ، نَأْكُلُ اَلْجَرَادَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn Abiy Awfaa amesema: “Tumepigana pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) vita saba, tunakula nzige.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1137.

وَعَنْ أَنَسٍ  فِي قِصَّةِ اَلْأَرْنَبِ  {قَالَ: فَذَبَحَهَا، فَبَعَثَ بِوَرِكِهَا إِلَى رَسُولِ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم فَقَبِلَهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Anas katika kisa cha sungura: “…akamchinja, akampelekea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) paja lake naye akalikubali.”[3] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1138.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم عَنْ قَتْلِ أَرْبَعِ مِنْ اَلدَّوَابِّ: اَلنَّمْلَةُ، وَالنَّحْلَةُ، وَالْهُدْهُدُ، وَالصُّرَدُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuwa wanyama wanne sisimizi, nyuki, hudihudi na kipwe (ndege).” [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

1139.

وَعَنْ اِبْنِ أَبِي عَمَّارٍ قَالَ: {قُلْتُ لِجَابِرٍ: اَلضَّبُعُ صَيْدُ هِيَ  ؟ قَالَ: نِعْمَ.‏ قُلْتُ: قَالَهُ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: نِعْمَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةَ ‏ وَصَحَّحَهُ اَلْبُخَارِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Ibn Abiy ‘Ammaar[4] amesema: “Nilimuuliza Jaabir fisi analiwa? Akasema Ndiyo.[5] Nikasema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema hivyo? Akasema ndiyo.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha Al-Bukhaariy na Ibn Hibbaan]

 

 

 

1140.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ  رضى الله عنه  ، أَنَّهُ سُئِلَ عَنْ اَلْقُنْفُذِ، فَقَالَ: ﴿ قُلْ لَا أَجدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَى طَاعِمٍ ﴾ ‏ فَقَالَ شَيْخٌ عِنْدَهُ: سَمِعْتَ أَبَا هُرَيْرَةَ يَقُولُ: {ذَكَرَ عِنْدَ اَلنَّبِيِّ  صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: خِبْثَةَ مِنْ اَلْخَبَائِثِ"} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَأَبُو دَاوُدَ، وَإِسْنَادُهُ ضَعِيفٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Aliulizwa kuhusu nungu akasema kwa kusoma Aayah hii: (Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji…) Qur-aan 6: 145. Mzee mmoja aliye kwake akasema: ‘Nilimsikia Abuu Hurayrah anasema alitajwa mbele ya Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Ni mchafu miongoni mwa vichafu’.” [Imetolewa na Ahmad na Abuu Daawuwd na isnaad yake ni dwaifu]

 

 

 

1141.

وَعَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم عَنْ اَلْجَلَّالَةِ وَأَلْبَانِهَا} أَخْرَجَهُ اَلْأَرْبَعَةِ إِلَّا النَّسَائِيُّ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ

Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kula mnyama anayekula uchafu na kunywa maziwa yake.”[6] [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

 

 

 

1142.

وَعَنْ أَبِي قَتَادَةٌ  رضى الله عنه  {فِي قِصَّةِ اَلْحِمَارِ اَلْوَحْشِيِّ فَأَكَلَ مِنْهُ اَلنَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abiy Qataadah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema katika kisa cha punda milia: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamla.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1143.

وَعَنْ أَسْمَاءِ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {نَحَرْنَا عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم فَرَساً، فَأَكَلْنَاهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Asmaa bint Abiy Bakr (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) tulichinja farasi na tukamla.”[7] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1144.

وَعَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {أَكُلَّ اَلضَّبِّ عَلَى مَائِدَةِ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Kenge aliliwa katika meza ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).”[8] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1145.

وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عُثْمَانَ اَلْقُرَشِيُّ  رضى الله عنه  {أَنَّ طَبِيباً سَأَلَ رَسُولَ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم  عَنْ اَلضِّفْدَعِ يَجْعَلُهَا فِي دَوَاءٍ، فَنَهَى عَنْ قَتْلِهَا} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Uthmaan Al-Qurashiyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Kuwa tabibu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ)  kuhusu chura kumfanya dawa. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akakataza kuuwa chura.”[9] [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Al-Haakim]

 

[1] Hadiyth hii inatoa maelezo kwamba kila mnyama mwenye kula mnyama na mwenye chonge ni haraam kuliwa. Vivyo kwa ndege anayenyofoa kiwindwa chake na kutumia ukucha ndege wa aina hiyo ni haraam kuliwa.

[2] Punda wa porinini (Pundamilia) ni halaal kuliwa.

[3] Sungura ni halaal kwa mujibu wa ‘Ulamaa wengi.

[4] Huyu ni ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Abdillaah bin Abuu ‘Ammaar Al-Qurayshiy Al-Makkiy. Alikuwa ni Mwenye Taqwa na An-Nasaaiy anamthibitisha kuwa ni madhubuti.

 

[5] Hadiyth inaonesha kuwa kumla fisi kumeruhusiwa. Kulingana na baadhi ya Maimaam (kama vile Shaafi’y) ni halaal. Wengine kama Hanafiy wanaona kuwa ni haraam. Sababu ya kuwa kwake ni haraam ni kuwa anapenda kula nyama ya mwana Aadam na kuichimbia chini.

[6] Katika lugha ya Kiarabu Jallaala ina maana ya wanyama wenye kula kwenye vinyaa, uchafu, awe mnyama huyo ni ngamia jike, ng’ombe au mbuzi. Hata ikiwa ni halaal kutumia nyama au maziwa yake, hili ni jambo lenye tofauti ya rai kati ya Wanazuoni tokea awali. Baadhi ya Wanazuoni wanaona kwamba ni halaali na wengine wakiona kuwa ni haraam. Mnyama ataonekana kuwa ni Jallaala ikiwa kiasi kikubwa cha chakula chake ni uchafu wa mwana Aadam. Ama ikiwa kiwango kikubwa cha chakula chake ni kinachoruhusiwa basi hatoingia katika kundi hili la Jallaala.

[7] Kuna Hadiyth iliyotangulia kabla ya hii ikisisitiza kuwa kula farasi ni halaal. Na hadiyth hii inathibitisha jambo hilo hilo.

[8] Tunajifunza katika baadhi ya Hadiyth kuwa Dhabbu (mburukenge) analiwa, pamoja na kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwenyewe hakumla, lakini Maswahaba wake walimla mbele yake katika meza yake. Alialikwa kumla lakini hakushiriki. Hakuwakataza watu kumla. Wanazuoni wanataja katika maandiko yao kuwa ni chukizo la Tanzihi (vile vilivyokuwa chini ya daraja la makatazo).

 

[9] Tunajifunza katika Hadiyth hii kuwa ni haraam kuuwa chura na kadhalika kumla.

Share