01-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Vyakula: Mlango Wa Kuwinda Na Kuchinja

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَاب اَلْأَطْعِمَةِ

Kitabu Cha Vyakula

 

بَاب اَلصَّيْدِ وَالذَّبَائِحِ

01-Mlango Wa Kuwinda Na Kuchinja

 

 

 

 

 

1146.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {"مَنِ اتَّخَذَ كَلْباً، إِلَّا كَلْبَ مَاشِيَةٍ، أَوْ صَيْدٍ، أَوْ زَرْعٍ، اِنْتَقَصَ مِنْ أَجْرِهِ كُلَّ يَوْمٍ قِيرَاطٌ" } مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kufuga mbwa isipokuwa mbwa wa kuwinda au wa mifugo au wa kulima[1] hakika kila siku anapunguziwa Qiyraatw kutoka katika ujira wake.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1147.

وَعَنْ عَدِيِّ بنِ حَاتِمٍ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {"إِذَا أَرْسَلَتَ كَلْبَكَ فَاذْكُرِ اسْمَ اَللَّهِ، فَإِنْ أَمْسَكَ عَلَيْكَ فَأَدْرَكْتَهُ حَيًّا فَاذْبَحْهُ، وَإِنْ أَدْرَكْتَهُ قَدْ قُتِلَ وَلَمْ يُؤْكَلْ مِنْهُ فَكُلْهُ، وَإِنْ وَجَدْتَ مَعَ كَلْبِكَ كَلْبًا غَيْرَهُ وَقَدْ قُتِلَ فَلَا تَأْكُلْ: فَإِنَّكَ لَا تَدْرِي أَيَّهُمَا قَتَلَهُ، وَإِنْ رَمَيْتَ سَهْمَكَ فَاذْكُرِ اسْمَ اَللَّهِ، فَإِنْ غَابَ عَنْكَ يَوْماً، فَلَمْ تَجِدْ فِيهِ إِلَّا أَثَرَ سَهْمِكَ، فَكُلْ إِنْ شِئْتَ، وَإِنْ وَجَدْتَهُ غَرِيقاً فِي اَلْمَاءِ، فَلَا تَأْكُلْ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَهَذَا لَفْظُ مُسْلِمٍ

Kutoka kwa ‘Adiyy bin Haatim[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema: “Unapomtuma mbwa wako, taja jina la Allaah[3] juu yake, akikukamatia (mnyama) nawe ukamkuta hai, basi mchinje na ukikuta ameuwa naye hakula chochote humo, basi kula, na ukikuta pamoja na mbwa wako kuna mbwa mwingine naye ameuwa basi usile, kwani hujui ni yupi aliyemuuwa. Na utakaporusha mshale wako taja Jina la Allaah. Itakapokupotea siku moja na (ukalipata halafu) usikute ila athari ya mshale wako, kula ukipenda. Na atakapompata ameghariki kwenye maji, usile.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

1148.

وَعَنْ عَدِيٍّ قَالَ: {سَأَلْتُ رَسُولَ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم عَنْ صَيْدِ اَلْمِعْرَاضِ ‏ فَقَالَ: "إِذَا أَصَبْتَ بِحَدِّهِ فَكُلْ، وَإِذَا أَصَبْتَ بِعَرْضِهِ، فَقُتِلَ، فَإِنَّهُ وَقِيذٌ، فَلَا تَأْكُلْ"} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Adiyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) kuhusu kuwinda kwa Mi’raadhw (mshale). Akasema: ‘Utakapolenga katika ukali wake,[4] kula na utakapolenga kwa ubavu wake na ikauwa, basi mnyama huyo ni mawquwdha[5] usile.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1149.

وَعَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ  رضى الله عنه  عَنِ اَلنَّبِيِّ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {" إِذَا رَمَيْتَ بِسَهْمِكَ، فَغَابَ عَنْكَ، فَأَدْرَكْتَهُ فَكُلْهُ، مَا لَمْ يُنْتِنْ"} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abiy Tha’labah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Utakaporusha mshale wako ukakupotea[6] ukaukuta (umeua windo), basi lile maadam halikuvunda harufu mbaya.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1150.

وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَنَّ قَوْمًا قَالُوا لِلنَّبِيِّ  صلى الله عليه وسلم إِنَّ قَوْماً يَأْتُونَنَا بِاللَّحْمِ، لَا نَدْرِي أَذُكِرَ اِسْمُ اَللَّهِ عَلَيْهِ أَمْ لَا ؟ فَقَالَ: " سَمُّوا اَللَّهَ عَلَيْهِ أَنْتُمْ، وَكُلُوهُ"} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Watu walimuambia Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) watu wanatujia na nyama hatujui kama wametaja Jina la Allaah juu yake ama hawakutaja? Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: ‘Nyinyi tajeni Jina la Allaah juu yake na muile.”[7] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1151.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بنِ مُغَفَّلٍ الْمُزَنِيِّ  رضى الله عنه  {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم نَهَى عَنِ اَلْخَذْفِ، وَقَالَ: "إِنَّهَا لَا تَصِيدُ صَيْدًا، وَلَا تَنْكَأُ عَدُوًّا، وَلَكِنَّهَا تَكْسِرُ اَلسِّنَّ، وَتَفْقَأُ اَلْعَيْنَ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.‏ وَاللَّفْظُ لِمُسْلِمٍ

Kutoka kwa ‘Abdillaah bin Mughaffal Al-Muzaniyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza mtu kurusha kijiwe na akasema: ‘Kwani kurusha kijiwe[8] hakuwindi windo wala hakuui adui, lakini huvunja jino na kupofua.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la Muslim]

 

 

 

1152.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {"لَا تَتَّخِذُوا شَيْئاً فِيهِ اَلرُّوحُ غَرَضًا"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msichukue kitu chenye roho kulengea shabaha.” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1153.

وَعَنْ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ  رضى الله عنه  {أَنّ امْرَأَةً ذَبَحَتْ شَاةً بِحَجَرٍ، فَسُئِلَ اَلنَّبِيُّ  صلى الله عليه وسلم عَنْ ذَلِكَ، فَأَمَرَ بِأَكْلِهَا} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Ka’b bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Mwanamke mmoja alichinja mbuzi kwa jiwe. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaulizwa kuhusu hilo akaamuru kuliwa kwake.”[9] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

1154.

وَعَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ  رضى الله عنه  عَنِ اَلنَّبِيِّ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {"مَا أُنْهِرَ اَلدَّمُ، وَذُكِرَ اِسْمُ اَللَّهِ عَلَيْهِ، فَكُلْ لَيْسَ اَلسِّنَّ وَالظُّفْرَ، أَمَّا اَلسِّنُّ، فَعَظْمٌ، وَأَمَّا اَلظُّفُرُ: فَمُدَى اَلْحَبَشِ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Raafi’ bin Khadiyj (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kinachomwaga damu na Jina la Allaah likatajwa juu yake, kula. Isipokuwa jino na kucha.[10] Ama jino ni mfupa. Na ama kucha ni kisu cha Wahabeshi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1155.

وَعَنْ جَابِرِ بنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم أَنْ يُقْتَلَ شَيْءٌ مِنَ اَلدَّوَابِّ صَبْرًا} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza mnyama kuuwawa kwa kutesa.”[11] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1156.

وَعَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {" إِنَّ اَللَّهَ كَتَبَ اَلْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا اَلْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا اَلذِّبْحَةَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، وَلْيُرِحْ ‏ ذَبِيحَتَهُ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Shaddaad bin Aws (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakika Allaah Ameandika hisani juu yake kila jambo. Mnapouwa, uweni kwa namna nzuri, na mnapochinja chinjeni kwa uzuri. Mmoja wenu akinoe kisu chake na amuondolee mashaka mnyama anayemchinja.”[12] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1157.

وَعَنْ أَبِي سَعِيدٍ اَلْخُدْرِيِّ  رضى الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ  صلى الله عليه وسلم {"ذَكَاةُ اَلْجَنِينِ ذَكَاةُ أُمِّهِ"} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Abiy Sa’iyd Al-Khudriyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kumchinja mtoto tumboni ni kwa kumchinja mama yake.”[13] [Imetolewa na Ahmad na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

1158.

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ اَلنَّبِيَّ  صلى الله عليه وسلم قَالَ: {" اَلْمُسْلِمُ يَكْفِيهِ اِسْمُهُ، فَإِنْ نَسِيَ أَنْ يُسَمِّيَ حِينَ يَذْبَحُ، فَلْيُسَمِّ، ثُمَّ لِيَأْكُلْ"} أَخْرَجَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَفِي إِسْنَادِهِ مُحَمَّدُ بنُ يَزِيدَ بنِ سِنَانٍ، وَهُوَ صَدُوقٌ ضَعِيفُ اَلْحِفْظِ

وَأَخْرَجَهُ عَبْدُ اَلرَّزَّاقِ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ إِلَى اِبْنِ عَبَّاسٍ، مَوْقُوفًا عَلَيْهِ

وَلَهُ شَاهِدٌ عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ فِي "مَرَاسِيلِهِ" بِلَفْظِ: {"ذَبِيحَةُ اَلْمُسْلِمِ حَلَالٌ، ذَكَرَ اِسْمَ اَللَّهِ عَلَيْهَا أَوْ لَمْ يَذْكُرْ"} وَرِجَالُهُ مُوَثَّقُونَ

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muislam linamtosha jina lake, akisahau BismiLLaah wakati wa kuchinja, basi aseme BismiLLaah kisha ale.”[14] [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy]

Katika Hadiyth hii kuna mpokezi hifadhi yake ni dhaifu ambaye ni Muhammad bin Yaziyd bin Sinaan[15] ni mkweli mwenye udhaifu wa kuhifadhi.

Abdur-Razzaaq ameipokea kwa isnaad sahihi ikinasibishwa kwa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas ikiwa ni Marfuw’.

Ina ushahidi kwa Abuu Daawuwd katika Maraasil kwa tamshi: “Chinjo la Muislam ni halaal, ataje Jina la Allaah wakati wa kuchinja ama asitaje.” Wapokezi wake ni madhubuti.

 

[1] Kwa sababu zisizokuwa za kuwinda na kuchunga vitu, ni haraam kumfuga mbwa kama mnyama wa nyumbani. Qiraatw ni kitu chenye thamani kubwa.

[2] ‘Adiyy bin Haatim bin At-Ta’i na baba yake walikuwa mashuhuri kwa ukarimu wao. Alimtembelea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwaka wa 7 HIjriyyah. Yeye pamoja na watu wake walithibitisha Uislam wao zaidi wakati wa Ar-Ridda. Zakkaah ya kwanza kumfikia Abuu Bakr ilikuwa kutoka kwa ‘Adiyy na watu wake. Alihudhuria ufunguzi wa Madain na alikuwa pamoja na ‘Aliy wakati wa vita vya Al-Jamaal, alifariki mwaka 120 Hijriyyah akiwa na miaka 68.

 

[3] Kuwinda kwa sababu ya kutafuta chakula au kuuza ni ruhusa. Ama ikiwa hilo linafanyika kwa sababu ya kutembea, kufurahi na kupoteza muda haitakiwi. Ni ruhusa kutumia mbwa au wanyama wengine kwa ajili ya kuwindia. Hata hivyo, kuna mambo mawili yanayotawala jambo hili: Kwanza unapomtuma mbwa wako unataja Jina la Allaah na pili, mbwa aliyetumwa anatakiwa yule aliyefundishwa kuwinda. Ikiwa mbwa yule kamla yule aliyemkamata anakuwa si halaal kwako kwani atakuwa amejiwindia na hakukuwindia.

[4] Moja katika hukumu ya uhalaal wa kuliwa kwa kiwindo ni kuwa ikiwa mnyama amekufa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali, basi ni halaal kuliwa ama ikiwa amekufa kwa kupigwa na kitu kikafa (kisichokuwa na ncha) usile kwani kitakuwa kimekufa kwa kupigwa.

 

[5] Yaani mnyama anayekufa kwa kupigwa na kitu kama vile fimbo au jiwe bila ya kuchinjwa.

[6] Ikiwa mnyama amepigwa mshale, kisha akakimbia usimuone na baadae ukakuta amekufa katika maji, hairuhusiwi kuliwa. Hata hivyo, ikiwa mnyama huyo huyo amepatikana akiwa hai, anatakiwa achinjwe. Ikiwa amekufa amelala chini na hana majeraha mengine zaidi ya mshale wako, ni halaal kumla. Ama akikutwa na jeraha lingine lisilokuwa la mshale wako basi ni haraam kumla.

 

[7] Hadiyth hii inatoa kanuni ya msingi kuwa mwana Aadam hakuna hakika kuwa nyama fulani si halaal, huna haja ya kusema kuwa si halaal maadamu huna hakika, na haswa zaidi ikiwa inatoka kwa Muislam.

 

[8] Hadiyth inaonesha kuwa vijiwe vinavyokusudiwa hapa ni vile vidogo visivyokuwa na manufaa.

[9] Mafundisho tuyapatayo katika Hadiyth hii yanaonesha kuwa ni halaal kwa mwanamke kuchinja kwa masharti kuwa: (a) Awe ni Muislam (b) Kabla ya akuchinja ataje Jina la Allaah kwa kusema BismiLLaah Allaahu Akbar.

[10] Kitu chochote chenye ncha kali (mbali na ukucha, mfupa au meno) ambayo itafanya damu ya mnyama kutiririka katika mwili wake, ni halaal kutumika kuchinjia.

 

[11] Katika lugha ya Kiarabu Swabr ina maana mbili: (a) kumuuwa mnyama kwa kumzuilia na maji au kufa kwa njaa, (b) Kumtumia mnyama kama kitu cha kulengea shabaha au kumtumia katika mazoezi ya kulenga shabaha. Yote haya ni haraam.

[12] Hata kama ni mtu anatakiwa kuuwawa basi anatakiwa auwawe kwa haraka bila kupata masumbuko yoyote ili afe kwa haraka.

[13] Hadiyth hii inaonesha kuwa kichanga kinafuata hukumu ya mama yake. Ikiwa mama ni halaal basi na kilicho ndani yake kinafuata hukumu hiyo. Ikiwa kichanga katika tumbo la mama ni hai basi atachinjwa kwa mujibu wa Wanazuoni.

 

[14] Ikiwa Muislam hakutaja Allaahu Akbar kwa makusudi wakati wa kuchinja basi nyama ile inakuwa ni haraam. Kama atakuwa amesahau basi ni halaal. Na hii ndio rai ya Wanazuoni.

[15] Huyu ni Abuu ‘Abdillaah alikuwa katika kabila la At-Tamiym. Abuu Haatim anamuelezea: ‘Hakuwa makini katika Hadiyth lakini pamoja na hayo alikuwa Mwenye Taqwa.’ Abuu Daawuwd anamuelezea: ‘Si wa kutegemewa’ na An-Nasaaiy anasema: ‘Hakuwa madhubuti.’ Ama Ibn Hibbaan amemtaja kuwa alikuwa Ath-Thiqah (kuwa alikuwa madhubuti). Alikufa mwaka 220 Hijriyyah.

Share