02-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Zuhd Yake: Akiomba Du’aa Kuambatanishwa Na Masikini Kufishwa Nao Na Kufufuliwa Nao

 Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

02-Zuhd Yake:

Akiomba Du’aa Kuambatanishwa Na Masikini Kufishwa Nao Na Kufufuliwa Nao

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiomba Du’aa ya kuambatanishwa daima na mafakiri na masikini, kufishwa nao na kufuliwa nao kwa sababu hali ya Masikini kawaida ni hali duni ambayo haina mafao ya dunia sawa na maisha ya mtu mwenye sifa ya Zuhd. Akiomba du’aa:

 

اللَّهُمَّ أَحْيِنِي مِسْكِينًا وَأَمِتْنِي مِسْكِينًا وَاحْشُرْنِي فِي زُمْرَةِ الْمَسَاكِينِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ

 ‏ 

Ee Allaah Nijaalia uhai wa umaskini na nifishe nikiwa maskini na nifufue pamoja na kundi la masaakini Siku ya Qiyaamah.” [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah]

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akathibitisha kuwa wengi wa makaazi ya Jannah (Peponi) watakuwa ni Masikini na Mafakiri:

 

 

عن ابن عباس وعِمْرَانَ بن الحُصَيْنِ رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ: (( اطَّلَعْتُ في الجَنَّةِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا الفُقَرَاءَ ، وَاطَّلَعْتُ في النَّارِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا النِّسَاءَ )) متفقٌ عَلَيْهِ من رواية ابن عباس ، ورواه البخاري أيضاً من رواية عِمْرَان بن الحُصَيْن .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas na 'Imraan Ibn Al-Huswayn (رضي الله عنهما)   kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)     amesema: "Nilichungulia Jannah nikaona watu wake wengi ni mafakiri. Na nikatizama Motoni nikaona watu wake wengi ni wanawake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

 

 

Share