F-Misamiati Yenye Asili Ya Lugha Ya Kiarabu

 

Misamiati Yenye Asili Ya Lugha Ya Kiarabu

Alhidaaya.com

 

F

Neno

Maana

Kiarabu

fadhila

kumfadhilisha mtu, kumfanyia wema, ukarimu, hisani, jamala, amali au ‘ibaadah inayosababisha kuchuma thawabu.

فضل

fahamu

kufahamu

فهم

faharasa/faharisi

orodha, sherehe, elezo.

فهرس

fakhari, fahari

kuwa na fahari ya jambo zuri, huenda ikamaanisha fahari ya kiburi kutokana na kujionyesha.

فخر

fasili

 

 

 

1-pambanuo, fafanua, bainisha waziwazi, kugawa au kuainisha maaandiko katika mafungu, kushona kitambaa, fungu la maneno, kutenganisha, kuachisha

فصل

fasili

sherehi, tanzua, changanua, fafanua, eleza waziwazi. 

 

فصل

fauka

juu

 

فوق

faulu

kufaulu, mafanikio

فلاح

fazaika

mshtuko mkubwa unaomfanya mtu azimie

فزع

fidiya

kufidia jambo kama fidia ya anayeshindwa kutekeleza ibaadah fulani, au kufidia kutokana na kupindukia mipaka katika ‘ibaadah, mfano: kufidia kwa kulisha maskini kwa ambaye hawezi swawm ya Ramadhwaan.

فدية

fikiri

kufikiri, kuwaza, kudhania.

فكر

fisadi

ufisadi

فساد  فسد

furahi

kufurahi. Katika Qur-aan huenda ikamaanisha kufurahi kwa kawaida au kufurahi kwa kujigamba kama kisa cha Qaaruwn katika [Suwrah Al-Qaswasw Aayah 76]

فرح

furkani

pambanuo, bainisho la haki na batili.

فرقان

futahi

kufungua, kupata ushindi wa nchi.

فتح

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share