022-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hajj Aayah 39: أذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّهَ عَلَى نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

 

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

022-Suwrah Al-Hajj Aayah 39

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّـهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٤٠﴾

Wameruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na kwamba Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru. Ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki isipokuwa kwa kuwa wanasema: Rabb wetu ni Allaah. Na lau ingelikuwa Allaah Hawakingi watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangelivunjwa mahekalu na makanisa, na masinagogi na Misikiti inayotajwa humo Jina la Allaah kwa wingi. Na bila shaka Allaah Atamnusuru yeyote yule anayenusuru Dini Yake. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika.[Al-Hajj: 39-40]

 

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أَحْمَدَ الزُّبَيْرِيُّ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ الْبَطِينِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ لَمَّا أُخْرِجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم مِنْ مَكَّةَ قَالَ رَجُلٌ أَخْرَجُوا نَبِيَّهُمْ فَنَزَلَتْ ‏:‏  أذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّهَ عَلَى نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ * الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِنْ دِيَارِهِمْ بِغَيْرِ حَقٍّ ‏ ‏ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم وَأَصْحَابُهُ ‏.‏

 

Ametuhadithia Muhammad bin Bash-shaar, ametuhadithia Abu Ahmad Az-Zubayriyy, ametuhadithia Sufyaan, kutoka kwa Al-A’mash, kutoka kwa Muslim Al-Batwan, kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr, amesema: Pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotolewa Makkah, mtu mmoja alisema: Wamemtoa Nabiy wao. Ikateremka:

 

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾

Wameruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na kwamba Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru.

 

الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ

Ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki

 

Yaani Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake. [Al-Bukhaariy]

 

Pia,

 

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ الأَزْرَقُ، قَالَ حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ الْبَطِينِ ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ لَمَّا أُخْرِجَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم مِنْ مَكَّةَ قَالَ أَبُو بَكْرٍ أَخْرَجُوا نَبِيَّهُمْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ لَيَهْلِكُنَّ ‏.‏ فَنَزَلَتْ ‏ أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا وَإِنَّ اللَّهَ عَلَى نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ‏ فَعَرَفْتُ أَنَّهُ سَيَكُونُ قِتَالٌ ‏.‏ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ فَهِيَ أَوَّلُ آيَةٍ نَزَلَتْ فِي الْقِتَالِ ‏.‏

 

Ametuhadithia Is-Haaq Al-Azraq] ametuhadithia Sufyaan toka kwa Al-A-‘amash toka kwa Muslim Al-Batwiyn toka kwa Sa’iyd bin Jubayr toka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: “Alipotolewa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   )   toka Makkah, Abu Bakr alisema: Wamemtoa Nabiy wao,

إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ

Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.

 

Hakika wataangamia. Hapo ikateremka:

 

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾

Wameruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na kwamba Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru.

[Al-Hajj (22:39)]

 

Akasema Abu Bakr: “Tunajua kuwa vitatokea vita”.

 

Ibn ‘Abbaas amesema: “Hii ndio Aayah ya kwanza kushuka kuzungumzia vita”.

 

 [Al-Imaam Ahmad   katika Mujallad wa Kwanza ukurasa 216, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy][1]

 

 


[1]

Wapokezi wa Hadiyth ni wapokezi wa As-Swahiyh (Isnaad yao imekharijiwa na Al-Bukhaariy au Muslim). At-Tirmidhiy ameikhariji na ameihasinisha katika Mujallad wa Nne ukurasa wa 151,  pia An-Nasaaiy katika Mujallad wa Sita ukurasa wa tatu, pia Ibn Jariyr katika Mujallad wa Saba ukurasa 172, pia At-Twabaraaniy katika Al-Mu-‘ujam wal Awaail, na vilevile Ibn Hibaan katika Mawaarid Adh-Dhwam-aan. Al-Haafidh Ibn Kathiyr ameinasibisha kwa Ibn Abiy Haatim katika Mujallad wa Tatu ukurasa wa 225, na Al-Haakim ameikusanya katika Mujallad wa Pili kurasa za 66, 246, na 390, na Mujallad wa Tatu ukurasa wa saba. Amesema kwa sharti ya Mashekhe wawili wote, na Adh-Dhahabiy amemnyamazia.
Kisha imeonekana kuwa kauli yenye nguvu ni kuifanya Mursal. Kwani At-Tirmidhiy, kwa uhakiki wa Ibraahiym ‘Atw-wah, amesema: Ameisimulia ‘Abdul Rahmaan bin Mahdiy na wengineo toka kwa Sufyaan ikiwa Mursal, na imetajwa kupitia kwa Ibn Az-Zubayr toka kwa Sufyaan ikiwa Mursal”.

 

Imetajwa kuwa Mawswuwl na Ibn Jariyr katika Mujallad wa Kumi na Saba ukurasa wa 172 kupitia kwa Qays bin Ar-Rabiy’i toka kwa Al-A-‘amash.

 

Na Al-Haakim ameisimulia katika Mujallad wa Tatu ukurasa wa saba kupitia kwa Shu-‘ubah akiwa mshiriki wa Sufyaan, lakini roho haitulii kwa mipwekeko ya Al-Haakim kutokana na kuwa mwingi wa mazigazi.

 

Halafu Al-Haafidh amemkuta Ad-Daaraqutwniy ameitaja katika Al-‘Ilal katika Mujallad wa Kwanza ukurasa wa 214 na kusema: Hiyo ni Hadiyth anayoisimulia Ath-Thawriy toka kwa Al A-‘amash toka kwa Muslim Al-Batwiyn toka kwa Sa’iyd bin Jubayr toka kwa Ibn ‘Abbaas.

Nayo imekhitalifiwa. Is-Haaq Al-Azraq na Wakiy’u wameifanya Mawswuwl toka kwa riwaayah ya mwanaye Sufyaan toka kwake na Al-Ashja’iyy toka kwa Ath-Thawriy.

Wengine wameifanya Mursal, na Ibn ‘Abbaas hakutajwa. Na Al-Firyaaniy ameisimulia toka kwa Qays bin Ar-Rabiy’i toka kwa Al-A-‘amash ikiwa Mawswuwl.

 

Na  kwa haya tunajua kuwa Hadiyth kuwa Mursal ndio mwelekeo wenye nguvu.

 

Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi

 

 

Share