Kababu Za Kuku Katika Sosi Ya Nyanya

Kababu Za Kuku Katika Sosi Ya Nyanya

Vipimo Vya Kababu                                             

Kidari cha kuku -  1 kilo

kitunguu saumu(thomu/galic)na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Kitunguu kilichokatwa vipande vidogo - 1

Pilipili mbichi - 1

Pilipili manga -  1 kijiko cha chai

Bizari upendayo -  1 kijiko cha chai

Siki - 1 kijiko cha supu

Mayai -    4 – 5

Mafuta -  Kiasi ya kukaangia  

Sosi

Mafuta -  3 vijiko vya supu

Vitunguu vilivyokatwa (chopped) -  2

Nyanya zilizosagwa - 3

Nyanya ya kopo - 1

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Chumvi  - kiasi

Kotmiri iliyokatwa (chopped)  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kababu 

  1. Chemsha kidari cha kuku kwa siki, thomu, kitunguu kilichosagwa, pilipili mbichi bizari zote na kufunika kipikike bila ya maji hadi kikauke.
  2. Tia katika mashine ya kusagia (blender) na usage bila ya kuta maji, kitasagika wenyewe.
  3. Tia katika bakuli na upige mayai na kuchanganya. Mchanganyiko uwe unaweza kufanya viduara vya kababu. Kama umekuwa laini ongeza mayai.
  4. Katika karai tia mafuta kiasi kidogo tu ya kuweza kugeuza geuza kababu zipikike.
  5. Epua na weka katika sufuria. 

Sosi 

  1. Kaanga vitunguu kisha tia nyanya, nyanya ya kopo, pilipili manga, chumvi na endelea kukaanga iwe sosi.
  2. Tia kotmiri, kisha mwagia katika sufuria iliyokuwemo kababu.
  3. Pika katika moto mdogo kababu zitokote kidogo hadi ziwive vizuri.
  4. Epua na pakua katika bakuli, mwagia kotmiri kidogo.

 

 

Share