Haleem Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan

AttachmentSize
Image icon Halim Nyama Mbuzi pakistani.jpg45.73 KB

Haleem Ya Nyama Mbuzi - Bokoboko La Pakistan

 

Vipimo

Nyama ya mbuzi au ng’ombe ya mafupa - 2 LB

Mchanganyiko wa dengu (hadesi, mchele, chooko, ngano, dengu n.k au nunua ya tayari iliyokwisha changanywa -   2  Vikombe

Kitungu maji (vikate vidogo) -  1

Mafuta -   ¼ Kikombe

Nyana kata ndogo ndogo  -    1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawazi iliyosagwa -  1 Kijiko cha supu

Bizari ya haleem  -   2 vijiko vya supu

Nyanya ya kopo  -   2  vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha nyama na chumvi ½ kijiko mpaka iive, toa mafupa.
  2. Chemsha mchanganyiko wa dengu mpaka ziive.
  3. Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu vilainike, tia thomu na tangawizi, *bizari ya haleem, nyanya ya kopo. Kaanga mpaka iwive.
  4. Tia nyama iliyowiva na supu yake kidogo.
  5. Tia mchanganyiko wa dengu tia kwenye mashine ya kusaga (blender), saga na ile supu ya nyama isagike vizuri
  6. Mimina kwenye sufuria changanya, tia ndimu kidogo, acha moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 15.
  7. Tia katika bakuli, pambia kwa vitunguu vilivyokaangwa vya rangi ya hudhurungi vikavu, pilipili mbichi (ukipenda) na kotmiri, ikiwa kuliwa.  

* Bizari ya haleem unaweza kutengeneza mwenyewe kama vile garama masala na bizari nzima ya pilau (uzile), bizari ya gilgilani (mbegu za kotimiri), paprika.

 

 

 

Share