Juisi Ya Embe

Juisi Ya Embe

 

 

Vipimo

Maembe yaliyoiva - 2

Mtindi (yogurt) - 2 Vikombe vya chai

Maziwa - 1 Kikombe cha chai

Asali au Sukari - ¼ Kikombe cha chai

Maji ya ndimu - ½ Kipande

Barafu - 12 vipande

Mdalasini ya unga - kidogo

 

Namna Ya Kutayarisha

  1. Ambua maembe kisha ukate kate vipande.
  2. Weka vipimo vyote isipokuwa mdalasini, kwenye mashine ya kusagia (blender).
  3. Saga hadi ilainike.
  4. Mimina kwenye gilasi na unyunyize mdalasini na itakuwa tayari.

 

Share