Pudini Ya Mkate, Jibini Na Siagi

Pudini Ya Mkate, Jibini Na Siagi

Vipimo

Slesi za mkate - 8

Jibini ya malai (cream cheese) - 3 Vijiko vya supu

Siagi - Kiasi

Maziwa - 2 vikombe

Maziwa ya kuvukiza (evaporated milk) - 1/4  Kikombe

Mayai - 5

Sukari - 5 vijiko vya supu

Vanilla - 1 kijiko cha supu

Zabibu kavu - kiasi kidogo

Namna ya kutayarisha na kupika 

  1. Paka jibini na siagi ueneze vizuri katika slesi za mkate.
  2. Funika moja juu ya mwenziwe kisha kata slesi za mkate ziwe vipande vya pembe tatu. 
  3. Zipange kwenye bakuli la kupikia katika oveni.
  4. Pasha moto maziwa kidogo tu, tia sukari na vanilla.
  5. Piga mayai katika kibakuli kidogo kisha changanya katika maziwa.
  6. Mwagia maziwa juu ya slesi za mkate.
  7. Tupia zabibu, kisha tia katika oveni upike katika moto wa 350º kwa muda wa dakika 45 au zaidi kidogo hadi pudini iwive igeuke rangi.
  8. Epua na tayari kuliwa.

Vidokezo: 

Pudini hii huliwa ikiwa dafu dafu, hivyo inafaa siku za baridi.

Ikiwa huna jibini ya malai unaweza kutia siagi pekee.

 

 

                                                       

 

Share