04-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake: Kulingania Wanafiki, Makafiri Na Kuwasamehe Wanapomtukana

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake:

 

04- Kulingania Wanafiki, Makafiri Na Kuwasamehe Wanapomtukana

 

Alhidaaya.com

 

 

Katika hikma zake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ilikuwa ni kuwasamehe wanafiki, washirikina na makafiri pindi wanapomtukana au kumfanyia isthizai, na katika kisi hiki kinaingia pia hikma yake ya kufuata ushauri wa Swahabi aliyemshauri awasamehe hao waovu waliomfanyia ufidhuli Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم).

 

 

حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، أَخْبَرَنَا هِشَامٌ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، قَالَ أَخْبَرَنِي أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم رَكِبَ حِمَارًا عَلَيْهِ إِكَافٌ، تَحْتَهُ قَطِيفَةٌ فَدَكِيَّةٌ، وَأَرْدَفَ وَرَاءَهُ أُسَامَةَ بْنَ زَيْدٍ وَهْوَ يَعُودُ سَعْدَ بْنَ عُبَادَةَ فِي بَنِي الْحَارِثِ بْنِ الْخَزْرَجِ، وَذَلِكَ قَبْلَ وَقْعَةِ بَدْرٍ حَتَّى مَرَّ فِي مَجْلِسٍ فِيهِ أَخْلاَطٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُشْرِكِينَ عَبَدَةِ الأَوْثَانِ وَالْيَهُودِ، وَفِيهِمْ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ، وَفِي الْمَجْلِسِ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ رَوَاحَةَ، فَلَمَّا غَشِيَتِ الْمَجْلِسَ عَجَاجَةُ الدَّابَّةِ خَمَّرَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ أَنْفَهُ بِرِدَائِهِ ثُمَّ قَالَ لاَ تُغَبِّرُوا عَلَيْنَا‏.‏ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ وَقَفَ فَنَزَلَ، فَدَعَاهُمْ إِلَى اللَّهِ وَقَرَأَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنَ فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أُبَىٍّ ابْنُ سَلُولَ أَيُّهَا الْمَرْءُ لاَ أَحْسَنَ مِنْ هَذَا، إِنْ كَانَ مَا تَقُولُ حَقًّا، فَلاَ تُؤْذِنَا فِي مَجَالِسِنَا، وَارْجِعْ إِلَى رَحْلِكَ، فَمَنْ جَاءَكَ مِنَّا فَاقْصُصْ عَلَيْهِ‏.‏ قَالَ ابْنُ رَوَاحَةَ اغْشَنَا فِي مَجَالِسِنَا، فَإِنَّا نُحِبُّ ذَلِكَ‏.‏ فَاسْتَبَّ الْمُسْلِمُونَ وَالْمُشْرِكُونَ وَالْيَهُودُ حَتَّى هَمُّوا أَنْ يَتَوَاثَبُوا، فَلَمْ يَزَلِ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يُخَفِّضُهُمْ، ثُمَّ رَكِبَ دَابَّتَهُ حَتَّى دَخَلَ عَلَى سَعْدِ بْنِ عُبَادَةَ فَقَالَ ‏ "‏ أَىْ سَعْدُ أَلَمْ تَسْمَعْ مَا قَالَ أَبُو حُبَابٍ ‏"‏‏.‏ يُرِيدُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ أُبَىٍّ قَالَ كَذَا وَكَذَا قَالَ اعْفُ عَنْهُ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَاصْفَحْ فَوَاللَّهِ لَقَدْ أَعْطَاكَ اللَّهُ الَّذِي أَعْطَاكَ، وَلَقَدِ اصْطَلَحَ أَهْلُ هَذِهِ الْبَحْرَةِ عَلَى أَنْ يُتَوِّجُوهُ فَيُعَصِّبُونَهُ بِالْعِصَابَةِ، فَلَمَّا رَدَّ اللَّهُ ذَلِكَ بِالْحَقِّ الَّذِي أَعْطَاكَ شَرِقَ بِذَلِكَ، فَذَلِكَ فَعَلَ بِهِ مَا رَأَيْتَ، فَعَفَا عَنْهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم‏

 

 

Amesimulia ‘Urwah bin Az-Zubayr kuwa Usaamah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)  alimhadithia: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  alipanda punda, mgongoni kwake kuna tandiko, chini yake kuna makhemeli (aina ya nguo laini) iliyotenegenezwa Fadak na nyuma yake amempakia Usaamah bin Zayd, naye anaenda kumuona Sa‘d bin ‘Ubaadah, katika Bani Haarith bin Al-Khazraj, na hiyo ilikuwa kabla ya Vita vya Badr. Mpaka akapita katika kikao kilicho na mchanganyiko wa Waislamu na mushrikina, wapagani na Mayahudi; na kati yao alikuwepo ‘Abdullaah bin Ubayy bin Saluwl na katika kikao kuna ‘Abdullaahi bin Rawaahah. Kikao kilipofunikwa na vumbi lililotimuliwa na wanyama. Abdullaaa, alifunika pua yake kwa utandiyo wake, kisha akasema: “Msitutimulie vumbi! [akimkusudia Nabiy صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم]”. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akawasalimia, kisha akasimama akateremka akawalingania kwa Uislamu na akawasomea Qur-aan. ‘Abdullaah bin Ubayy bin Saluwl akasema: “Wee mtu wee! Hivi hakuna kizuri zaidi ya hiki? Ikiwa unachokisema ni kweli, basi usituudhi katika mabaraza yetu, na rudi kambini kwako na atakayekujia miongoni mwetu muelezee”. Ibn Rawaahah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) akasema: “Tujie katika mabaraza yetu, kwani sisi tunayapenda hayo.” Basi wakaanza kugombana kati ya Waislamu, mushrikina na Mayahudi, mpaka wakataka kurukiana; Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaendelea kuwatuliza. Kisha akapanda mnyama wake, mpaka akafika kwa Sa‘d bin ‘Ubaadah akasema: “Ee Sa‘d! Haukuyasikia aliyoyasema Abu Hubaab?” Anamkusudia ‘Abdallaah bin Ubayy. Amesema kadhaa wa kadhaa. Akasema (Sa‘d): “Ee Rasuli wa Allaah, msamehe, wa-Allaahi Allaah Amekupa Alichokupa, na watu wa mji huu walikusudia kumpa ufalme na wamfunge kilemba. Allaah Alipolikataa hilo kwa haki Aliyokupa, likawa limemkera sana, kwa hilo akashtushwa na kuduwaa, sababu hiyo akakufanyia uliyoyaona”. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akamsamehe. [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share