07-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake: Hakumpuuza Mtu Aliyenongo’na Naye

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hikmah Zake:

 

07-Hakumpuuza Mtu Aliyenongo’na Naye 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Katika hikma zake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alibakia kumsikiliza mtu ambaye alimnongo’neza tena ilikuwa Msikitini na akaendelea kumsikiliza huku Swahaba zake (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ) wakisubiri hadi wakapatwa na usingizi kisha ilipoadhiniwa Iqaamah ya Swalaah wakainuka kuswali na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم):

 

 

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ، عَنْ أَنَس ٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ أُقِيمَتِ الصَّلاَةُ وَرَجُلٌ يُنَاجِي رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَمَا زَالَ يُنَاجِيهِ حَتَّى نَامَ أَصْحَابُهُ، ثُمَّ قَامَ فَصَلَّى‏.‏

 

Amesimulia Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)  kwamba: Swalaah ilikimiwa na ilhali mtu mmoja anamnong’oneza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Aliendelea kumnong’oneza mpaka Swahaba zake wakalala, na baada ya hapo Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alisimama na kuswali. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Kuomba Rukhsa]

 

 

 

 

 

Share