10-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuoga Ni Bora Zaidi

 

   

Kwa vyovyote, kukoga josho (ghuslu) kunapendeza zaidi kuliko kufanya wudhuu katika hali kama hizi.  Abu Raafi' amesimulia kwamba:

 

 

أنَّ النَّبي صلى الله عليه وسلم طاف ذَاتَ يَوْمٍ علَى نِسائِهِ يَغْتَسِلُ عِنْدَ هَذِهِ وَعِنْدَ هَذِهِ. قال فَقُلْتُ لَهُ: يا رسولَ الله ألاَ تجْعَلُهُ غُسْلاً وَاحِداً؟ قال: ((هَذَا أزْكَى وَأطْيَبُ وَأطْهَرُ))

 

 

"Mtume aliwazungukia (aliwaingilia) wake zake usiku mmoja, akikoga katika kila nyumba ya mmoja wao". Yeye (msimuliaji) alimuuliza Mtume, je, si ungeliweza kukoga mara moja tu?' (yaani mwishoni). Mtume akajibu: ((Hivi ni utakaso zaidi, usafi na bora))[1]

 





[1] Abu Daawuud, An-Nasaaiy: Hasan katika "Al-Ishraah" na wengineo

 

 

 

 

Share