16-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Makatazo Ya Jimai (Kitendo Cha Ndoa) Wakati Wa Hedhi

Imekatazwa kwa mume kufanya jimai (kitendo cha ndoa) na mkewe wakati yuko kwenye hedhi. Hii ni dhahiri kutokana na Aayah ya Qur-aan:

 

((وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُواْ النِّسَاء فِي الْمَحِيضِ وَلاَ تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىَ يَطْهُرْنَ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللّهُ إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ))

 

"Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka watwaharike. Wakishatoharika (na kujitoharisha) basi waendeeni Alivyokuamrisheni Allaah. Hakika Allaah Huwapenda wanaotubu na Huwapenda wanaojitakasa" (Al-Baqarah 2:222)

 
Vile vile kuna Hadiyth kuhusu mas-ala haya, miongoni mwa hizo ni:

Kwanza:

 

((مَنْ أَتَى حَائِضاً  أَوْ امْرَأَةً فِي دُبُرهَا، أَوْ كَاهِناً؛ فَصَدَقَهُ بِمَا يَقُول  فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أنْزلَ عَلىَ مُحَمَّد)) 

 

"Yeyote atakayejimai (kufanya kitendo cha ndoa) na mwanamke mwenye hedhi, au kwa kutumia njia ya nyuma, au kumwendea kahini (mtabiri) na kuamini aliyoambiwa, basi amekufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad"[1]

 

Pili:

 

عن أنَسِ بنِ مَالِكٍ، قال: إنَّ الْيَهُودَ كَانَتْ إذَا حَاضَتْ مِنْهُم المَرْأةُ أخْرَجُوهَا مِنْ الْبَيْتِ وَلَمْ يُؤَاكِلُوهَا وَلَمْ يُشَارِبُوهَا وَلَمْ يُجَامِعُوهَا في الْبَيْتِ فَسُئِلَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَنْ ذَلِكَ، فأنْزَلَ الله تَعَالَى ذِكْرُهُ: ((وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ المَحِيضِ قُلْ هُوَ أذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ في المَحِيضِ)) إلَى آخِرِ الآيَةِ. فقال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((جَامِعُوهُنَّ في الْبُيُوتِ، وَاصْنَعُوا كُلَّ شَيْىءٍ غَيْرَ النِّكَاحِ)). فقالت الْيَهُودُ: مَا يُرِيدُ هَذَا الرَّجُلُ أنْ يَدَعَ شَيْئاً مِنْ أمْرِنَا إلاَّ خَالَفَنَا فِيهِ. فَجَاءَ أُسَيْدُ بنُ حُضَيْرٍ وَعَبَّاد بنُ بِشْرٍ إلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فقالا: يارسولَ الله صلى الله عليه وسلم إنَّ اليَهُودَ تَقُولُ كَذَا وكَذَا، أفَلاَ نَنْكِحَهُنَّ في المَحِيضِ؟ فَتَمَعَّرَ وَجْهُ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم حَتَّى ظَنَنَّا أن قَدْ وُجِدَ عَلَيْهِمَا، فَخَرَجَا، فَاسْتَقْبَلَتْهُمَا هَدِيَّةٌ مِنْ لَبَنِ إلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَبَعَثَ في آثَارِهِمَا فَسَقاهُما، فَظَنَنَّا أنَّهُ لَمْ يَجِدْ عَلَيْهِمَا   

 

Kutoka kwa Anas ibn Maalik ambaye amesema: "Anapokuwa mmoja wa wanawake wao wako katika hedhi, Mayahudi walikuwa wakimuweka nje ya nyumba, na huwa hawali, hawanywi wala kulala naye katika nyumba. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipoulizwa jambo hili, Allaah سبحانه وتعالى Aliteremsha Aayah "Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi" Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema:  "Kuweni nao katika nyumba na mfanye kila kitu nao isipokuwa jimai pekee". Mayahudi wakasema: 'Mtu huyu hataki kuacha lolote tulifanyalo ila alipinge'.  Akaja Usayd ibn Khudhwayr na 'Abbaad ibn Bishr wakasema: 'Ee Mjumbe wa Allaah, hakika Mayahudi wanasema kadha wa kadha, je, kwa nini tusifanye jimai wakati wa hedhi (ili tutofautiane na Mayahudi)?' Uso wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ukabadilika hadi kwamba walifikiri amewakasirikia. Wakaondoka, na walipokuwa wanatoka, wakaona zawadi ya maziwa imeletwa kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamtuma mtu kuwafuata na kuwapa kinywaji cha maziwa, wakatambua kuwa hakuwakasirikia".[2]

 

 

[1] Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na wengineo: Swahiyh

[2] Muslim, Abu 'Awwaanah na Abu Daawuud

Share