17-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kafara (Malipo) Ya Mtu Anayejimai Katika Hedhi

 

 

Yeyote aliyeteleza, akafanya kosa la jimai na mke wake wakati yuko katika hedhi na kabla ya kuwa ametoharika, itampasa atoe thamani ya uzito wa dinari ya dhahabu au kiasi cha gramu 4.25 (kwa uhakika zaidi ni 4.2315) au nusu yake.

 
Hii ni kutokana na Hadiyth iliyopokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Abbaas عنهما رضي الله kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika uhusiano wa mtu atakayemuingilia mkewe wakati yuko kwenye hedhi kama ifuatavyo:

 

عبد الله ابن عباسٍ رضي الله عنهما  فـي الَّذي يأتـي امرأَتَهُ وَهِيَ حَائِضٌ قال: ((يَتَصَدَّقُ بدينارٍ أو نصفِ دينارٍ))

"Mwache atoe dinari moja katika sadaka au nusu ya dinari"[1]
 

 


[1] At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, At-Twabaraaniy na wengineo: Swahiyh

Share