18-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Yanayoruhusiwa Anapokuwa Katika Hedhi

Mume anaruhusiwa kustarehe na mkewe kwa njia yoyote isipokuwa sehemu zake za siri anapokuwa katika Hedhi. Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu jambo hili:

Kwanza:

((...اصْنَعُوا كُلَّ شَيْءٍ إِلاَّ النِّكَاحَ))

"…fanyeni kila kitu isipokuwa jimai pekee"[1]

 
 

Pili:

عن عَائِشَةَ رضي الله عنها ، قَالَتْ:  كانَ رَسُولُ اللَّهِ، يَأْمُرُ إِحْدَانَا إِذا كَانَتْ حَائِضاً أَنْ تَتَّزِرََ ثُمَّ يُضَاجِعُهَا زَوْجُهَا وَقالَتْ مَرَّةً: يُبَاشِرُهَا.

Kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Tulipokuwa katika siku zetu (hedhi) Mtume alikuwa akituamrisha tuvae nguo kiunoni ili mume aweze kulala naye". Na akasema (mama wa waumini ‘Aaishah) pia …"Mumewe aweze kumkumbatia na kumpapasa".[2]

 

Tatu:

عن بَعْضِ أزْوَاجِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قالَتْ: إنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إذَا أرَادَ مِنَ الْحَائِضِ شَيْئاً ألْقَى عَلَى فَرْجِهَا ثَوْباً [ ثم صنع ما أراد]  

Kutoka kwa mmoja wa wake zake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipokuwa anataka kitu (kufurahi naye) kutoka kwa wake zake siku za hedhi, alikuwa anaweka nguo katika sehemu zake za siri kisha hufanya anavyotaka".[3]

 

 


[1] Muslim, Abu 'Awwaanah na Abu Daawuud

[2] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

[3] Abu Daawuud: Swahiyh

Share