23-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Afanye Nini Siku Ya Pili Baada Ya Ndoa

Inapendekezeka kwa mume kwenda kwa jamaa zake ambao walikuja kumtembelea nyumbani kwake, siku ya pili kuwaamkia na kuwaombea. Wao pia inapendekezeka kumfanyia hivyo hivyo, kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo iliyosimuliwa na Anas رضي الله عنه:

 

أَوْلَم رَسُولُ الله إذ بنى بِزَيْنَبْ فَأَشْبَعَ الْمُسْلِمِينَ خُبْزاً وَلَحْماً ثُمَّ خَرَجَ إِلَى أُمَّهَاتِ الْمُؤْمِنِينَ فَسَلَّمَ عَلَيْهِنَّ وَدَعَا لَهُنَّ وَسَلَّمْنَّ عَلَيْه وَدعونَ لَهُ فَكَانَ يَفْعَلْ ذَلِكَ صَبِيحَة بنائه

"Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alialika karamu asubuhi ya usiku wa harusi yake na mama wa waumini Zaynab, ambayo aliwalisha Waislamu mikate na nyama mpaka wakashiba. Kisha akaenda kwa Mama za Waumini (wake zake wengine) akawasalimia na kuwaombea, nao wakarudisha (maamkizi na Du'aa) kwa upole. Hivi ndivyo alivyokuwa akifanya asubuhi baada ya usiku wa ndoa"[1]

 

 

[1] Ibn Sa'ad na An-Nasaaiy: Swahiyh

Share