35-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kutokubali Mwaliko Katika Shughuli Zenye Maasi Ndani Yake

 

 

Hairuhusiwi kuhudhuria shughuli alizoalikwa mtu ambazo zina mambo ya kumuasi Allaah سبحانه وتعالى ila ikiwa mtu atakwenda kwa nia ya kuwaeleza watu ubaya huo na kujaribu kuuondosha. Akifaulu kuondosha au kuzuia basi anaweza kubakia, na kama akishindwa basi aondoke. Kuna Hadiyth kuhusu mas-ala haya, miongoni mwa hizo ni:

 

Kwanza:

عَنْ عَلِيَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: صَنَعْتُ طَعَامَاً فَدَعَوْتُ رَسُولَ اللَّهِ فَجَاءَ فَرَأَىٰ تَصَاوِيرَ، فَرَجَعَ قَال:  فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا رَجَعَكَ بِأَبِي أَنْتَ وَأُمي ؟ قَالَ: ((إِنَّ فِي الْبَيْتِ سِتْرَاً فِيهِ تَصَاوِيرُ، وَإِنَّ المَلاَئِكَةَ لاَ تَدْخُلُ بَيْتَاً فِيهِ تَصَاوِيرُ))

 
Imetoka kwa 'Aliy رضي الله عنه ambaye amesema: "Nilitayarisha chakula kisha nikamualika Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم Alipokuja na akaona picha katika nyumba akageuka kuondoka. Nikamuambia: Ewe Mjumbe wa Allaah, jambo gani lililokurudisha, baba yangu na mama yangu wawe fidia yako? Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Kuna pazia katika nyumba hii ambalo lina picha, na Malaika hawaingii katika nyumba yoyote yenye picha))[1]

 

Pili:

عن عائشة أَنَّهَا اشْتَرَتْ نُمْرُقَةً فِيهَا تَصَاوِيرُ. فَلَمَّا رَآهَا رَسُولُ اللّهِ قَامَ عَلَى الْبَابِ فَلَمْ يَدْخُلْ. فَعَرَفْتُ، أَوْ فَعُرِفَتْ، فِي وَجْهِهِ الْكَرَاهِيَةُ. فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللّهِ أَتُوبُ إِلَى اللّهِ وَإِلَىٰ رَسُولِهِ. فَمَاذَا أَذْنَبْتُ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللّهِ : ((مَا بَالُ هٰذِهِ النُّمْرُقَةِ؟)) فَقَالَتِ: اشْتَرَيْتُهَا لَكَ. تَقْعُدُ عَلَيْهَا وَتَوَسَّدُهَا. فَقَالَ رَسُولُ اللّهِ : ((إِنَّ أَصْحَابَ هٰذِهِ الصُّوَرِ (  وفي رواية: إن الذين يعملون هذه التصاوير) يُعَذَّبُونَ يَوم الْقِيَامة وَيُقَالُ لَهُمْ: أَحْيُوا مَا خَلَقْتُمْ)) ثُمَّ قَالَ: ((إِنَّ الْبَيْتَ الَّذِي فِيهِ الصُّوَرُ لاَ تَدْخُلُهُ الْمَلاَئِكَةُ)).

 

 

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye alisema kwamba alinunua mito ambayo ilikuwa ina picha. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipoiona alisimama mlangoni na hakuingia. Nikatambua kuchukizwa kwake sana usoni mwake. Nikasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, ninatubu kwa Allaah na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Wake, nimefanya nini?" Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akauliza, ((Mto gani huu?)) Nikasema: Nimekununulia wewe ili uukalie na uutumie kama mto. Akasema: ((Hakika watu picha hizi [katika riwaaya nyingine] ((wale wanaochora picha hizi) wataadhibiwa siku ya Qiyaamah na wataambiwa: Vipeni uhai katika vile mlivyoviumba!)) Kisha akasema:  ((Nyumba ambayo inayo picha kama hizi hawaingii Malaika)) ’Aaishah akasema: Hakuingia tena hadi nilivyoondosha mto".[2]

 

Tatu:

 

(( مَنْ كَانَ يُؤْمِن بالله وَالْيَوْمِ الآخِر؛ فَلاَ يَقْعُدَنَّ عَلَى مَائِدَةٍ يُدَار عَلَيْها بِالْخَمْر )).

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema, ((Yeyote anayemuamini Allaah na Siku ya Mwisho, asikae katika meza inayozungushwa ulevi))[3]

Desturi ya vitendo vya Salaf (kizazi cha mwanzo cha Waislamu) ilikuwa ndivyo hivi ambavyo tumevieleza hapa. Kuna mifano mingi lakini tutataja mifano michache tu:

 

Kwanza:

 

 

عن أَسْلَـمَ مولـى عُمَرَ أَنَّ عُمَرَ بنَ الـخطابِ رضي الله عنه حينَ قَدِمَ الشأْمَ فَصَنَعَ لهُ رجلٌ من النَّصَارَى طعاماً، فقالَ لِعُمَرَ: إنِّـي أُحِبُّ أَنْ تَـجِيْئَنِـي وتُكْرِمَنِـي أَنْتَ وأصحابُكَ، وهو رجلٌ من عظماءِ الشأْمِ، فقالَ لهُ عُمَرُ رضي الله عنه: إنَّا لا نَدْخُـلُ كَنَائِسَكُمْ من أجلِ الصورِ الَّتِـي فِـيْهَا، يعنـي التـماثـيلَ

 

Kutoka kwa Aslam mkombolewa wa 'Umar  kwamba 'Umar ibnul Khatw-Twaab alikuja Ash-Shaam. Mtu mmoja katika Manaswara alitayarisha chakula na akamuambia 'Umar: 'Nitapenda uje kwangu ili unipe heshima [muwe wageni wangu wa heshima] pamoja na Swahaba zako'. (Huyo mtu alikuwa ni mkuu miongoni mwa watu wa Ash-Shaam). 'Umar akamuambia, 'Hatuingii makanisa yenu kwa sababu ya mapicha yaliyomo humo.'[4]

 

Pili:

 
 

عن أبـي مسعودٍ أَنَّ رجلاً صَنَعَ لهُ طعاماً فَدَعَاهُ، فقالَ: أَفِـي البـيتِ صورةٌ، قالَ: نَعَمْ، فأَبَى أَنْ يَدْخُـلَ حتَّـى كَسَرَ الصورةَ، ثم دَخَـلَ

Imetoka kwa Abu Mas'uud 'Uqba bin 'Aamir kwamba mtu mmoja alimtayarishia chakula kisha akamualika. Abu Mas'uud akamuuliza yule mtu: 'Je kuna picha katika nyumba?" Yule mtu alimjibu: 'Ndio'. Hivyo Abu Mas'uud alikataa kuingia hadi picha zilipovunjwa kisha akaingia.[5]

 
Tatu:

 

  قَالَ الإِمَام الأَوْزاعِي: لاَ نَدْخُل وَلِيمَةُ فِيهَا طبل وَلاَ معْزَاف   

 

Imaam Al-Awzaa'iy amesema: "Hautuingii katika karamu iliyo na ngoma au ala za muziki"[6]

 

 

 

 

 

[1] Ibn Maajah na Abu Ya'laa

[2] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

[3] Ahmad na At-Tirmidhiy: Swahiyh

[4] Al-Bayhaaqiy: Swahiyh

[5] Al-Bayhaaqiy: Swahiyh

[6] 'Abdul-Hasan Al-Harbiy katika 'Al-Fawaaidul Muntaqaat (4/3/1/) ikiwa Isnaad Swahiyh kutoka kwake

 

 

Share