36-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Yanayopendezwa Kufanywa Na Waalikwa

 

 

Mambo mawili yanapendekezwa kwa wale wanaohudhuria shughuli waliyoalikwa:


Jambo La
Kwanza: Du’aa Kumuombea Mwenyeji


Inampasa amuombee Du'aa mwenyeji wake baada ya kumaliza kula, Du'aa ambazo zimenukuliwa kutoka kwa Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم nazo ziko aina mbali mbali:

 


Kwanza:

عَنْ عَبْدُالله بِنْ بسر ، يَحدثْ أَنَّ أبَاهُ صَنَعَ لِلنَّبِيِّ طَعَاماً، فَدَعَاهُ فأجَابَهُ، فَلَمَّا فَرَغَ قَال: ((اَللَّهُمَّ اْرَحَمْهُمْ وَاغْفِرْ لَهُمْ وَبَارِكْ لَهُمْ فِيمَا رَزَقْتَهُمْ)).

 

Imetoka kwa 'Abdullah ibn Bisr baba yake alitayarisha chakula kwa ajili ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kisha akamualika. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye aliitikia na akahudhuria. Alipomaliza kula, Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alisema ((Ewe Allaah, Waghufurie, Warehemu na Wabarikie yale Uliyowaruzuku)) (Allaahumma-Ghfir-Lahum War-hamhum, wa Baarik-Lahum Fiy-Maa Razaqtahum)[1]


Pili:

عن المقداد بن الأسود ،قال: قدمت أنا وصاحبان لي على رسول الله صلى الله عليه وسلم فأصابنا جوع شديد، فتعرضنا للناس فلم يُضِفْنا أحد، فانطلق بنا رسول الله صلى الله عليه وسلم إلى منزله وعنده أربع أَعْنُزٍ فقال لي: ((يا مِقْدادُ جَزِّىءْ أَلْبانَها بَيْنَنَا أَرْباعاً)) فكنت أجزئه بيننا أرباعاً [فيشرب كل إنسان نصيبه، ونرفع لرسول الله صلى الله عليه وسلم نصيبه]  فاحتبس رسول الله صلى الله عليه وسلم ذات ليلة فحدثت  أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قد أتى بعض الأنصار، فأكل حتى شبع، وشرب حتى روي، فلو شربت نصيبه، فلم أزل كذلك حتى قمت إلى نصيبه فشربته، ثم غطيت القَدح، فلما فرغت أخذني ما قدم وما حدث، فقلت: يجيء رسول الله صلى الله عليه وسلم جائعاً ولا يجد شيئاً فتسجَّيتُ،  قال: وعلي شملة من صوف كلما رفعت على رأسي خرجت قدماي، وإذا أرسلت على قدمي خرج رأسي، قال:] [وجعل لا يجيئني النوم]   وَجعلت أحدث نفسي، [قال: وأما صاحباي فناما]،    فبينا أنا كذلك، إذ دخل رسول الله صلى الله عليه وسلم فسلم تسليمة، يُسْمِعُ اليقظان ولا يُوقظ النائم، [ثم أتى المسجد فصلى]،   ثم أتىٰ القدح فكشفه فلم ير شيئاً، فقال: ((اللهمَّ أَطْعِمْ مَنْ أَطْعَمَني واسْقِ مَنْ سَقاني)) واغتنمت الدعوة،   [فعمدت إلى الشملة فشددتها علي]  فقمت إلى الشفرة فأخذتها، ثم أتيت الأعنز فجعلت اجتسها أيها أسمن، فلا تمر يدي على ضرع واحدة إلا وجدتها حافلاً،  [فعمدت إلى إناء لآل محمد ما كانوا يطعمون أن يحلبوا فيه]،  فحلبت حتى ملأت القَدَح،  ثم أتيت [به]   رسول الله صلى الله عليه وسلم، [فقال: ((أما شربتم شرابكم الليلة يا مقداد؟)) قال:]    فقلت: اشرب يا رسول الله، فرفع رأسه إليّ فقال: ((بعضُ سَوْآتِكَ ـ يا مِقْدادَ ـ ما الخبر؟)) قلت: اشرب ثم الخبر، فشرب حتى روى، ثم ناولني فشربت،  فلما عرفت أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قد روي وأصابتني دعوته، ضحكت، حتى ألقيت إلى الأرض، فقال: ((ما الخَبَرْ؟)) فأخبرته فقال: ((هٰذِهِ بَرَكَةٌ نَزَلَتْ مِنَ السَّماءِ فَهَلاَّ أَعْلَمْتَني حَتَّى نَسْقِيَ صاحِبَيْنا)) فقلت: [والذي بعثك بالحق]،  إذاً أصابتني وإياك، البركة فما أبالي من أخطأت

 

Imetoka kwa Al-Miqdaad ibn Al-Aswad رضي الله عنه ambaye alisema: "Nilikwenda na rafiki zangu wawili kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم (Madiynah). Tulikuwa na njaa na tukaomba msaada kwa watu wengine, lakini hakuna aliyetupokea kuwa wageni wao. Kisha Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم alituchukua nyumbani kwake na huko kulikuwepo na mbuzi wanne. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliniambia, ((Ewe Miqdaad, gawa maziwa baina yetu mara nne)). Nikagawa maziwa katika sehemu nne. Kila mmoja akanywa kiasi chake, na tukampelekea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم sehemu yake. Usiku mmoja, Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم alikawia nje, nikaanza kuwaza akilini mwangu kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amekwenda kwa ma-Answaar na amekula mpaka ameshiba na amekunywa mpaka amekata kiu chake, basi kwa nini nisinywe sehemu yake? (kiasi chake cha maziwa) Ikaendelea hivyo hadi mwisho nikainuka na kunywa sehemu yake. Kisha nikafunika gilasi yake. Nilipomaliza, nikaanza kutia wasiwasi nilivyofanya, nikiwaza katika nafsi yangu kuwa sasa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم atakuja akiwa ana njaa na atakuta hakuna kitu. Nikajifunika blanketi la sufi. Nilipolivuta blanketi juu ya kichwa changu miguu yangu ilijitokeza na nilipojifunika miguu yangu, kichwa kilikuwa wazi hakikufunikwa. Sikuweza kulala, nikawa nawaza mambo katika nafsi yangu. Ama marafiki zangu wawili, walikuwa wameshalala. Nilibakia katika hali hii alipoingia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akanisalimia kwa sauti ya kusikika na mtu aliyekuwa macho, lakini ambayo isingelimuamsha aliyelala. Baada ya hapo akaenda msikitini na kuswali. Kisha akaijia gilasi na kuifungua lakini hakuona kitu ndani yake na akasema: ((Ewe Allaah Mlishe aliyenilisha na Mpe kinywaji yule anayenipa kinywaji)) (Allaahuuma Atw-'im Man Atw'amaniy Wasqi man Saqaaniy). Nikaamua kuchukua fursa ya Du'aa hii ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Nikachukua blanketi langu na nikalivaa kiunoni, nikachukua kisu kikubwa, nikawaendea mbuzi. Nikaanza kuwakagua kwa mikono yangu kutazama aliyenona kabisa ili nipate kumchinja kwa ajili ya Mjumbe wa Allaah lakini kila mikono yangu ikipita katika kila chuchu iliona kwamba zimejaa maziwa. Nikachukua chombo kilichokuwa cha watu wake wa nyumbani kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambacho hawakuweza kufikiria kuwa kitajaa maziwa nikaanza kukamua maziwa ya mbuzi hadi kikajaa. Kisha nikamletea Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye aliniambia, ((Hukunywa maziwa yako usiku huu ewe Miqdaad?)) Nikasema: 'Kunywa Ewe Mjumbe wa Allaah' Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akanyanyua kichwa chake na akasema, ((Ni aibu kwako ewe Miqdaad yaliyotokea)). Nikasema: 'Kunywa kwanza, kisha ndio habari. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akanywa mpaka akakata kiu chake kisha akanipa gilasi na nikanywa pia.


Nilipojua kwamba Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم ameshakata kiu chake na kwamba Du'aa yake imeshanihusu kuitumia nikaanza kucheka hadi nikaanguka chini kwa kicheko.

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Kuna nini?)). Nikamuelezea kisa chote. Akasema, ((Hii (yaani maziwa yasiyotegemewa) ni baraka kutoka mbinguni. Kwa nini usiniambie ili tungeliwapa pia rafiki zako sehemu? (ya hayo maziwa))). Nikasema: 'Naapa kwa Yule Ambaye Amekuleta kwa haki, madamu baraka zimekujia wewe na mimi, haikunishughulisha sana na kufikiria waliokosa maziwa haya'.[2]


Tatu:

 

عن أَنَسٍ أَوْ غيرِهِ  أن رسول الله صلى الله عليه وسلم [ كان يزور الأنصار، فإذا جاء إلى دور الأنصار جاء صبيان الأنصار يدورون حوله، فيدعوا لهم، ويمسح رؤوسهم ويسلم عليهم، فأتى إلى باب سعد بن عبادة فـ]   اسْتَأْذَنَ علـى سعدِ بنِ عُبَادَةَ رضي الله عنه فقالَ: ((السلامُ عَلَـيْكَ ورَحْمَةُ الله)) قال سَعْدٌ: وعلـيكَ السلامُ ورَحْمَةُ الله، ولـم يُسْمِعِ النبـيَّ حتَّـى سَلَّـمَ ثلاثاً، ورَدَّ علـيهِ سعدٌ ثلاثاً ولـم يُسْمِعْهُ، [وكان النبي صلى الله عليه وسلم لا يزيد فوق ثلاث تسليمات، فإن أذن له، وإلا انصرف]، فَرَجَعَ النبـيُّ، فاتَّبَعَهُ سعدٌ فقالَ: يا رسولَ الله بأَبِـي أنتَ ما سَلَّـمْتَ تسلـيـمةً إلاَّ وَهِيَ بأُذُنِـي، ولَقَدْ رَدَدْتُ علـيكَ ولـم أُسْمِعْكَ أَحْبَبْتُ أَنْ أَسْتَكْثِرَ من سَلاَمِكَ ومن البَرَكَةِ،  ثم دَخَـلُوا البـيتَ، فَقَرَّبَ لهُ زَبِـيباً، فَأَكَلَ نبـيُّ الله، فلـمَّا فَرَغَ قالَ: ((أَكَلَ طَعَامَكُمُ الأبرارُ، وصَلَّتْ عَلَـيْكُمُ الـملائكةُ، وأَفْطَرَ عِنْدَكُمُ الصائمونَ»))

Imetoka kwa Anas عنه رضي الله na wengineo, kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiwatembelea ma-Answaar. Kila alipokwenda nyumbani mwao watoto wao walikuwa wakija kumzunguka Naye hucheza nao na kuwapapasa vichwa vyao na kuwasalimia. Siku moja, alikuja mlangoni mwa Sa'ad ibn 'Ubaadah na akaomba ruhusa kuingia akisema: ((Assalaamu 'Alaykum)). Sa'ad akajibu 'Wa 'alaykumus salaam', lakini kwa sauti ambayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakuisikia. Ikafanyika hivyo mara tatu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakupata kuomba ruhusa kuingia zaidi ya mara tatu ikiwa hakupewa idhini ya kuingia, bali huondoka. Akaondoka Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Sa'ad akamfuata na akasema: 'Ewe Mjumbe wa Allaah, baba yangu na mama yangu wawe fidia yako, kila mara ulipotoa salaam, nilikupa idhini lakini sikutaka uisikie kwa sababu nilipenda kusikia salaam nyingine na baraka kutoka kwako. Kwa hiyo karibu Ewe Mjumbe wa Allaah. Kisha wakaingia nyumbani na kumkaribisha ale zabibu. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akala, alipomaliza alisema, ((Wale chakula chenu watu wema, na wawaombee Rehema Malaika na wafuturu kwenu waliofunga)) (Akala Twa'aamakumul-Abraar Wa Swallat 'Alaykumul-Malaaikatu Wa Aftwara 'Indakumus-Swaaimuun)[3]

 

Jambo La Pili: Du’aa Kuwaombea Bwana na Bibi Harusi


Jambo la pili linalopendekezeka kwa wale wanaohudhuria karamu ya harusi ni kuwaombea Du'aa bwana na bibi harusi wajaaliwe kheri na baraka. Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu mas-ala haya:


Kwanza:

 

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللّهِ عنهما قال:  هَلَكَ أَبِي وَتَرَكَ سَبْعَ  بَنَاتٍ (أَوْ قَالَ تِسْعَ ) فَتَزَوَّجْتُ امْرَأَةً ثَيِّباً. فَقَالَ لِي رَسُولُ اللّهِ ((يَا جَابِرُ! تَزَوَّجْتَ؟)) قَالَ قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: ((فَبِكْرٌ أَمْ ثَيِّبٌ؟)) قَالَ قُلْتُ: بَلْ ثَيِّبٌ، يَا رَسُولَ اللّهِ! قَالَ: ((فَهَلاَّ جَارِيَةً تُلاَعِبُهَا وَتُلاَعِبُكَ)) و في رواية: ((وَتُضَاحِكُهَا وَتُضَاحِكُكَ؟)) قَالَ قُلْتُ لَهُ: إِنَّ عَبْدَ اللّهِ هَلَكَ وَتَرَكَ تِسْعَ بَنَاتٍ (أَوْ سَبْعَ) وَإِنِّي كَرِهْتُ أَنْ آتِيَهُنَّ أَوْ أَجِيئَهُنَّ بِمِثْلِهِنَّ، فَأَحْبَبْتُ أَنْ أَجِيءَ بِامْرَأَةٍ تَقُومُ عَلَيْهِنَّ وَتُصْلِحُهُنَّ. قَالَ: ((فَبَارَكَ الّلهُ لَكَ)) أَوْ قَالَ لِي خَيْراً.

 
Imetoka kwa Jaabir ibn 'Abdullaah رضي الله عنه ambaye amesema: "Baba yangu alifariki na aliacha wasichana saba (au tisa). Nilimuoa mwanamke aliyekuwa thayyib [mjane] na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akaniuliza, ((Umeshaoa ewe Jaabir?)). Nikajibu, 'Ndio'. Akauliza tena, ((Je, ni bikra au mjane?)). Nikajibu, "Ni mjane". Akauliza, ((Kwa nini usingeoa msichana mdogo ambaye angelicheza nawe nawe ungelicheza naye?)) Katika riwaaya nyingine, ((na ambaye angelikuchekesha na ungelimchekesha)). Nikasema,  "Abdullaah amefariki na ameacha wasichana tisa [au saba] na sikupenda kuwaletea mke aliye sawa na wao kwa hiyo nimeoa mwanamke ambaye atakuwa na mas-uliya nao na kuwapa mafunzo vizuri". Mtume صلى الله عليه وآله وسلم   akasema, ((BarakAllaahu Laka)) (Allaah Akubariki) [au alisema jambo jema kwangu][4]


Pili:

 

وعن بريدة قال: قال نفر من الأنصار لعلي ـ رضي الله عنه ـ: عندك فاطمة ، فأتى رسول الله صلى الله عليه وسلّم (فَسَلَّم عليه ) فقال:  ((مَا حَاجَةُ ابنُ أَبي طَالِبٍ))   فقال: يا رسول الله، ذكرت فاطمة بنت رسول الله صلى الله عليه وسلّم، فقال: ((مَرْحَباً وأَهْلاً)) لم يزد عليها. فخرج علي بن أبي طالب على أولئك الرهط من الأنصار ينتظرونه، فقالوا: ما وراءك؟ قال: ما أدري غير أنه قال لي: ((مَرْحَباً وأَهْلاً)) قالوا: يكفيك من رسول الله صلى الله عليه وسلّم إحداهما، أعطاك الأهل والمرحب. فلما كان بعدما زوجه قال: ((يا عَلِيُّ إِنَّه لا بُدَّ لِلْعَرُوسِ مِنْ وَلِيْمَةٍ)) قال سعد: عندي كبش، وجمعَ له من الأنصار أَصْوُعاً من ذرة، فلما كانت ليلة البناء قال: ((لا تُحْدِثْ شَيْئاً حَتَّيه تَلْقَانِي)) فدعا رسول الله صلى الله عليه وسلّم بماء فتوضأ منه، ثم أفرغه عليَّ فقال: ((اللهمَّ بَارِكْ فِيهِمَا وبَارِكْ لَهُمَا في بِنَائِهِمَا))

Imetoka kwa Buraydah رضي الله عنه ambaye amesema: "Baadhi ya ma-Answaar walimuambia 'Aliy: 'Unaye Faatwimah!' Kwa hiyo 'Aliy akaenda kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم 'Aliy alipomsalimia alisema, ((Unahitaji nini ewe mwana wa Abu Twaalib?)). 'Aliy Akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, Faatwimah mtoto wa Mjumbe wa Allaah ametajwa". Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Marhaban [karibu] na Ahlan)) [umo miongoni mwa familia])) kisha hakusema kitu zaidi. 'Aliy alirudi kwa kundi la ma-Answaar waliokuwa wakimsubiri na wakamuuliza imekuwaje. 'Aliy akasema: "Sijui amesema Marhaban na Ahlan". Wakasema, "mojawapo (ya maneno hayo mawili) kutoka kwa Mjumbe wa Allaah yangelitosheleza! Amekukaribisha kuwa mmoja katika wana familia. Kisha baada ya 'Aliy kumuoa Faatwimah, Mtume صلىالله عليه وآله وسلم akamuambia, ((Ewe 'Aliy, kila bwana harusi lazima afanye karamu)). Sa'ad akasema: "Mimi nina kondoo". Na kundi la ma-Answaar wakakusanya mahindi. Ulipofika usiku wa kuingia (usiku wa Ndoa), Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم alimuambia, ((Usifanye lolote hadi ukutane na mimi)). Kisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akaomba aletewe maji, akayatumia kwa wudhuu na akamwagia 'Aliy (yaliyobakia) huku akiomba, ((Ewe Allaah Wabariki hawa wawili na Wabariki katika kuingiliana kwao [ndoa yao]))[5]

 


Tatu:

عَنْ عَائِشَةَ ، قَالَتْ: تَزَوَّجَنِي النبي صلى الله عليه وسلم   فأتتني أمي فأدخَلَتني الدار، فَإِذَا نِسْوَةٌ مِنَ الأَنْصَارِ في البيت فَقُلْنَ: عَلَى الْخَيْرِ وَالْبَرَكَةِ، وَعَلَى خَيْرِ طَائِرٍ

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliponioa, mama yangu alikuja kwangu na akaniweka katika nyumba. Kuliwemo wanawake wa Answaar ndani ambao walisema: "(Ndoa) ya kheri na baraka, yaani ndoa yenye hadhi na kheri nyingi" ('Alal-Khayri Wal-Barakati Wa 'Ala Khayri Twaairiyn))[6]

 


Nne:

 

عن أبي هريرةَ ، عنِ النبيّ صلى الله عليه وسلّم أنَّهُ كانَ إذا رَفّأَ الإنسانَ إذا تزوج   قالَ: ((بارَكَ اللَّهُ لكَ وباركَ عليكَ وجمعَ بينكُمَا في خيرٍ))

 

Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه: "Kila mtu alipoanza kuishi na mkewe baada ya kumuoa, Mtume صلى الله عليه وآله وسلم   alikuwa akisema, "Allaah Akubariki na Abariki juu yako, na Awajumuishe katika kheri" (Baaraka Allaahu Laka Wa Baaraka Allaahu 'Alayka Wa Jama'a Baynakumaa Fiy Khayrin)[7]

 

 



 

[1] Ibn Abi Shaybah, Muslim na wengineo

[2] Muslim, Ahmad na wengineo

[3] Ahmad, Al-Bayhaaqiy na wengineo: Swahiyh

[4] Al-Bukhaariy na Muslim

[5] Ibn Sa' na At-Tirmidhiy: Hasan

[6] Al-Bukhaariy, Muslim na Al-Bayhaaqiy

[7] Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na wengineo: Swahihy

 

 

Share