38-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Bibi Harusi Anaweza Kuwahudumia Wanaume

 

 

Hakuna ubaya kwa bibi harusi kuwahudumia mwenyewe wageni madamu atakuwa amevaa mavazi ya Kiislamu na ikiwa hakuna mategemeo ya uovu.
Hii ni kutokana na Hadiyth iliyosimuliwa na Sahl ibn Sa'ad ambaye amesema:

 

لما عرَّسَ أبو أُسَيد الساعِدِيُّ دعا النبيَّ صلى الله عليه وسلم وأصحابَهُ فما صنَع لهم طعاماً ولا قدم إليهم إلا امرأتُهُ أمُّ أُسيد، بَلَّتْ   (وفي رواية: أنقعت)  تَمَراتٍ في تَوْر من حجارةٍ منَ الليل، فلما فَرَغَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم من الطعام أماثَتْه له فسقَتْهُ تتْحِفُه بذلك . (فَكَانَتِ امْرَأَتُهُ يَوْمَئِذٍ خَادِمَهُمْ. وَهْيَ الْعَرُوسُ)

 

"Abu Usayd As-Saa'idiy alipooa na siku ile alipomuingilia mkewe, alimualika Mtume صلى الله عليه وآله وسلم pamoja na Maswahaba zake. Hakuna aliyetayarisha chakula au kuwahudumia isipokuwa mkewe Ummu Asyad. Aliroweka tende katika bakuli la udongo usiku uliopita. Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم alipomaliza kula, alimpakulia na kumtunikia, hivyo mkewe akawa ndiye mwenye kuwahudumia wageni na alikuwa ndiye bi harusi"[1]

 


Mavazi ya Kiislamu ni yale yanayotakiwa kuvaliwa kisheria

 

Nayo ni lazima yatimize masharti manane yafuatayo:

 
1) Mwili wote ufunikwe isipokuwa uso na viganja vya mikono.

 
2) Nguo isiwe yenye mapambo;

 
3) Lazima iwe nzito kiasi isiwe yenye kuonyesha mwili;

 
4) Lazima iwe ya kupwaya na sio ya kubana hata ikaonyesha kiwiliwili chake;

 
5) Asijitie manukato;

 
6) Isishabihi vazi la kiume;

 
7) Isishabihi mavazi ya kikafiri;

 
8) Isiwe ya kujionyesha, maana kwamba isiwe kwa ajili ya kiburi kuwa ni vazi bora kuliko la mwingine.


Katika kitabu kingine cha Shaykh Al-Albaaniy "Hijaab Ya Mwanamke Wa Kiislamu Katika Qur-aan Na Sunnah" ametoa hoja na dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah kwa kila sharti hizo)

 

 

 



[1] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

Share