41-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Wajibu Wa Kuishi Mume Na Mkewe Kwa Huruma

 

 

Ni waajib wa Mume kuishi na mkewe katika hali njema kabisa na kuwa mpole kwake kwa yote Aliyoyaruhusu Allaah سبحانه وتعالى khaswa ikiwa mke ni mdogo kwa umri. Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu mas-ala haya:

 


Kwanza:

  قالَ رسُولُ اللّه صلى الله عليه وسلم ِ: ((خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لأَهْلِهِ، وَأَنَا خَيْرُكُمْ لاِهلِي))

   

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema, ((Mbora wenu ni yule ambaye ni mbora kwa wake zake, na mimi ni mbora wenu kwa wake zangu))[1]

 


Pili:

 

  قوله صلى الله عليه وسلم في خطبة حجة الوداع:  (( ...ألاَ واسْتَوْصُوا بالنِّسَاءِ خَيراً، فإنهن عَوانٌ عِنْدَكمْ لَيْسَ تَمْلِكُونَ مِنْهُنَّ شَيْئاً غَيْرَ ذلِكَ، إلاَّ أَنَّ يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ فَإِنْ فَعَلْنَ فَاهجُرُوهُنَّ في المضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ضَرْباً غَيْرَ مُبَرِّحٍ. فَإنْ أطَعْنكُمُ فَلاَ تَبْغُوا علَيْهِنَّ سَبِيلاً. أَلاَ إنّ لَكُمْ عَلَى نِسَائِكُم حَقّاً. ولِنسَائِكمْ عَلَيْكُمْ حَقاً. فَأَمَّا حَقكُّمْ عَلَى نِسَائِكُمْ فَلاَ يُوطِئنَ فُرُشكُمْ مَنْ تَكْرَهُونَ ولاَ يَأْذَنَّ في بُيُوتِكُمْ لِمَنْ تَكْرَهُونَ. ألاَ وحَقهُنَّ عَلَيْكُمْ أنْ تُحسِنُوا إِلَيْهِنَّ فِي كِسْوَتِهِنَّ وطَعَامِهِن))

 

Kauli ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika Hijjat Al-Wadaai, ((Sikilizeni! Wafanyieni wema wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu na hamuwamiliki zaidi ya hivyo.[2] Hamumiliki chochote kwao isipokuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Wakifanya hivyo basi muwahame katika malazi (msijamiane nao) wapigeni pigo lisiloumiza (yaani watieni adabu tu msiwaumize) Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika nyinyi mna haki kwao na wao wana haki kwenu. Ama haki yenu kwa wake zenu ni wasimruhusu mtu msiyempenda kukalia zulia lenu wala wasimruhusu mtu msiyempenda kuingia nyumbani mwenu. Naam, na haki zao kwenu ni kuwafanyia wema katika kuwapatia mavazi na chakula chao"[3]


Tatu:

 

 ((لا يفرك( أي لا يبغض ) مُؤْمِنٌ مُؤمِنَة، إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خَلْقاً رَضِيَ مِنْهَا آخر)) 

((Muumini mwanamume asimchukie Muumini mwanamke, ingawa anaweza kuchukia tabia moja (lakini) atapendekezewa na nyingine))[4]

 


Nne:

  ((أَكْمَلِ المؤمنينَ إيماناً أحْسَنُهُمْ خُلُقاً  وَخِيَاركُمْ خِيَاركُمْ لِنِسَائِكُمْ))

((Waumini waliokamilika kwa imani ni wale wenye tabia njema kabisa, na walio bora kabisa ni wale wanaowafanyia wema kabisa wanawake wao))[5]

 


Tano:

 

عَنْ عائِشَة رضي الله عنها قالت:  دَعانِي رسول الله صلى الله عليه وسلم (وَالْحَبَشَة يَلْعَبُونَ بِحرابِهِمْ في الْمَسْجِد)، (في يوم عيد)، فقال لي: ((يَا حميراء أَتُحِبِّينَ أَنْ تَنْظُرِي إِلَيْهْم؟)) فَقُلْتُ: نَعَمْ  (فأقامني وراءه)، فطأطأ لي منكبيه لأنظر إليهم، (فوضعت ذقني على عاتقه، وأسندت وجهي إلى خده)، فنظرت من فوق منكبيه ( وفي رواية: من بين أذنه وعاتقه ) (وهو يقول: ((دونك يا بني أرفده)) فجعل يقول: ((يا عائشة! ما شبعت!)) فأقول: لا، لأنظر منزلتي عنده) حتى شبعت(قالت: ومن قولهم يومئذ: أبا القاسم طيباً) وفي رواية:  (حتى إذا مللت، قال: ((حسبك؟)) قلت نعم، قال: ((فاذهبي))، وفي أخرى: ((قلت: لا تعجل، فقام لي، ثم قال : ((حسبك؟)) قلت: لا تعجل، (ولقد رأيته يرواح بين قدميه)، قالت: ما بي حب النظر إليهم، ولكن أحببت أن يبلغَ النساء مقامُه لي، ومكاني منه (وأنا جارية)، (فاقدروا قدر الجارية [العربة] الحديثة السن، الحريصة على اللهو)، [قالت: فطلع عمر، فتفرق الناس عنها والصبيان، فقال النبي صلى الله عليه وسلم : ((رأيت شياطين الإنس والجن فروا من عمر))،  قالت عائشة: قال صلى الله عليه وسلم يومئذٍ: ((لتعلم يهود أن في ديننا فسحة )). البخاري ومسلم وغيرهم.

 

Kutoka kwa mama wa waumini 'Aaishah kuwa alisema, "Siku ya 'Iyd Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuja kwangu wakati wa Habeshi (Wa-Ethiopia) walipokuwa wakicheza kwa kutumia mishale yao msikitini na kuniambia, ((Ewe mdogo mwekundu, unapenda kuwatazama?)) Nikajibu, Ndio. Kisha akanisimamisha nyuma yake na kuyateremsha mabega yake ili nipate kuwaona. Nikaweka kidevu changu mabegani mwake uso wangu ukiwa baina ya shavu lake. Nikawatazama kupitia kwenye mabega yake… huku akiniuliza mara kwa mara, ((Je, umetosheka?))  (kuwatazama) Nami niliendelea kusema: Bado, ili nijaribu kuona penzi lake kwangu hadi nilipotosheka". ‘Aaishah akasema: "Jambo moja walilosema siku hiyo ilikuwa ni: "Abu Al-Qaasim ni mwenye tabia njema". (Na katika riwaaya nyingine ilipokelewa kuwa alisema) "Nilipochoshwa na maonyesho, aliniuliza, ((Je, umetosheka?)) Nikajibu, "Usiniharakize". Kwa hiyo akaendelea kunisimamia. Aliponiuliza mara ya pili kama nimetosheka, nikamwambia tena asiniharakize. Nikamuona akibadilisha miguu yake kwa ajili ya machofu" ‘Aaishah akasema: "Sikuwa na hamu ya kuwatazama, bali nilitaka habari ziwafikie wanawake kuhusu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kunijali na kusimama kwa ajili yangu (ili wajue jinsi gani alivyokuwa akinijali) ingawa nilikuwa msichana, (Na hii ) ili wathamini hali ya msichana mdogo kwa umri mwenye kupenda burudani na mchezo". ‘Aaishah akasema: "Kisha 'Umar akaja na watu wakatawanyika mpaka watoto. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Nimewaona mashaytwaan wote wa kibinaadamu na majini wakimkimbia 'Umar)). ‘Aaishah akasema, Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema siku hiyo, ((Kwa hiyo Mayahudi wajue kuwa katika Uislamu kuna wasaa na ni Dini isiyokataza burudani na michezo??))[6]

 


Sita:

عنْ عَائِشَةَ،قَالَتْ: قَدِمَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ غَزْوَةِ تَبُوكَ أَوْ خَيْبَرَ وَفِي سَهْوَتِهَا سِتْرٌ فَهَبَّتِ الرِّيحُ فَكَشَفَتْ نَاحِيَةَ السَّتْرِ عنْ بَنَاتٍ لِعَائِشَةَ لُعَبٍ، فقَالَ: ((مَا هٰذَا يَا عَائِشَةُ؟)) قالَتْ بَنَاتِي، وَرَأَى بَيْنَهُنَّ فَرَسَا لَهُ جَنَاحَانِ مِنْ رِقَاعٍ، فقَالَ: ((مَا هٰذَا الَّذِي أَرَى وَسْطَهُنَّ؟)) قَالَتْ فَرَسٌ، قَالَ: ((وَمَا هٰذَا الَّذِي عَلَيْهِ؟)) قُلْتُ جَنَاحَانِ، قَالَ: ((فَرَسٌ لَهُ جَنَاحَانِ؟)) قَالَتْ أمَا سَمِعْتَ أَنَّ لِسُلَيْمانَ خَيْلاً لَهَا أَجْنِحَةٌ، قَالَتْ: فَضَحِكَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم حَتَّى رَأَيْتُ نَوَاجِذَهُ .

Kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها ambaye amesema "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alirudi kutoka vita vya Tabuuk au vya Khaybar. Kulikuwa na pazia chumbani kwake. Upepo ukapeperusha na ukainua pazia na kuonyesha sehemu ya chumba ambacho Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliona watoto wa sanamu aliokuwa akichezea ‘Aaishah. Akauliza, ((Nini hii ewe ‘Aaishah?)) Akajibu, "Watoto wangu wa kike".  (Waarabu walikuwa wakiwaita masanamu "watoto wa kike"). Aliona pamoja nao farasi mwenye mbawa mbili aliyetengenezwa kwa kitambaa.  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamuuliza tena mama wa waumini 'Aaishah, ((Na hii nini katikati?)). Akajibu, "Ni farasi". Akauliza tena, ((Na nini hivyo vilivyo juu ya farasi?)). 'Aaishah akajibu, "Mbawa mbili". Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Farasi mwenye mbawa mbili?)) ‘Aaishah akasema, "Je, hukusikia kuwa Nabii Sulayman alikuwa na farasi wenye mbawa?"  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم (baada ya kusikia hayo) alicheka mpaka nikayaona magego yake"[7]

 


Saba:

 

عن عائشةُ رضي الله عنها أَنَّهَا كانتْ معَ النبيِّ في سَفَرٍ وهي جاريةٌ، (قالت: لم أحمل اللحم، ولم أبدن)، فقالَ لأَصْحَابِهِ: ((تَقَدَّمُوا))، (فَتَقَدَّمُوا)، ثم قالَ: ((تَعَالَيْ أُسَابِقْكِ))، فَسَابَقْتُهُ فَسَبَقْتُهُ على رِجْلَيَّ، فلمَّا كانَ بَعْدُ، خرجتُ أيضاً مَعَهُ في سفرٍ، فقالَ لأَصْحَابِهِ: ((تَقَدَّمُوا))، ثم قالَ: ((تَعَالَيْ أُسَابِقْكِ))، ونسيتُ الَّذِي كانَ وقد حَمَلْتُ اللحمَ،[وبدّنت]، فقلتُ: وكيفَ أُسَابِقُكَ يا رسولَ اللَّهِ وأَنَا على هذِهِ الحالِ، فقالَ: ((لَتَفْعَلِنَّ))، فَسَابَقْتُهُ فَسَبَقَنِي، (فـجعل يضحك،) و فقالَ: ((هذِهِ بِتِلْكَ السَّبْقَةِ))

 

  
Kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah
عنها رضي الله kwamba alikuwa pamoja na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika safari naye akiwa ni msichana mdogo. (mama wa waumini 'Aaishah akielezea safari hiyo alisema), "Sikuwa mnene na wala sikuwa na mwili mkubwa". Wakati huo Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم aliwaambia Maswahaba wake, ((Tangulieni)). Walipotangulia na wakawa mbele yetu, Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم akaniambia, ((Njoo nishindane na wewe mbio)) Nikamshinda mbio za mguu. Baada ya muda kupita hivi, nikawa naye tena katika safari na akawaambia tena Maswahaba wake, ((Tangulieni)) Kisha akaniambia, ((Njoo nishindane na wewe mbio)). Nilisahau kabisa mashindano ya mbio ya mwanzo. Juu ya hivyo nilikuwa nimenenepa. Nikamuambia, "Nitakimbia vipi nami niko katika hali hii?" Akanijibu, ((Utashindana nami)). Nikakimbia naye akashinda mbio. Akaanza kucheka na kusema, ((Hii ni kulipiza ushindi wako wa mwanzo))[8]

 


Nane:

 

عن عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا إن كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ليؤتىٰ بالإناء فَأَشْرَبُ مِنْهُ وَأَنَا حَائِضٌ ثُمَّ  ثُمَّ يَأْخُذْهُ فَيَضَع فاهُ عَلَى مَوْضِع فيّ وَإنْ كُنْت لآخذ الْعَرَق فآكُل مِنْه، ثُمَّ يَأخُذه فَيَضَع فَاهُ عَلى مَوْضِع فيّ

 
Kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah
رضي الله عنها ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akiletewa gilasi ya maziwa ambayo nilikuwa nikinywa kwanza na huku niko katika hedhi. Kisha akiichukua gilasi na akiiweka mdomo wake pale nilipoweka mimi mdomo wangu na kunywa. Mara nyingine nilikuwa nikichukua kipande cha nyama na kukila kisha naye akikichukua na kuweka mdomo wake pale nilipokula mimi kisha hukila"[9]

 


Tisa:

عن جابر بن عبد اللَّه وجابر بن عمير رضَي اللَّهُ عنهُ   قالا: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((كُلُّ شَيْءٍ لَيْسَ فِيهِ ذِكْرِ اللَّهِ فَهُوَ (لغوٌ) وَسَهْوٌ وَلَعِبٌ إِلاَّ أَرْبَعَ (خصال): مُلاَعَبَةُ الرَّجُلِ امْرَأَتَهُ، وَتَأْدِيبُ الرَّجُلِ فَرَسَهُ، وَمَشْيَهُ بَيْنَ الهَدَفَيْنِ، وَتَعْلِيمُ الرَّجُلِ السبَاحَة

Kutoka kwa Jaabir ibn 'Abdillaah رضي الله عنه pamoja na Jaabir ibn 'Umar رضي الله عنه ambao wote wawili wameripoti kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema, ((Vitu vyote pasi na kumtaja Allaah ni upuuzi, usahaulifu na mchezo isipokuwa vitu vinne; mtu kucheza na mkewe, kumfundisha farasi, kutembea baina ya lengo lililokusudiwa, na kumfundisha mtu kuogelea))[10]

 



[1] At-Twahaawiy: Swahiyh

[2] Tuhfatul-Ahwadhiy Sharh At-Tirmidhiy 4/326 na Sharh Ibn Maajah 1/567

[3] At-Tirmidhiy na Ibn Maajah: Swahiyh

[4] Muslim na wengineo

[5] At-Tirmidhiy na Ahmad: Hasan

[6] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

[7] Abu Daawuud, An-Nasaaiy katika 'Al-Ishraah': Swahiyh)

[8] Al-Humaydiy, An-Nasaaiy katika 'Al-Ishraah', Abuu Daawuud na wengineo: Swahiyh

[9] Muslim, Ahmad na wengineo

[10] An-Nasaaiy katika 'Al-Ishraah' At-Twabaraaniy na wengineo

Share