Anaweza Kwenda Hajj Ikiwa Ana Deni La Swawm Za Ramadhwaan?

 

Anaweza Kwenda Hajj Ikiwa Ana Deni La Swawm Za Ramadhwaan?

 

 Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Ukiwa na deni la saumu ya Ramadhaan halafu Allaah akajalia deni lile hukuwahi kulipa mpaka imefikia wakti umeenda zako hijja jee inakuwaje?juu ya hijja yako?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Deni la Ramadhwaan lina wasaa na muda wa kulipa japokuwa ni vyema zaidi kulipa haraka iwezekanavyo na kutegemea kama udhuru uliokufanya usifunge siku kadhaa za Ramadhaan umeondoka. Siku ulizokosa kufunga unaweza kulipa baada ya ‘Iydul Fitwr (1 Shawwal) hado kabla ya Ramadhwaan ya mwaka unaofuata (yaani mwezi wa Sha‘baan).

 

Swawm na Hijjah ni ‘Ibaadah mbili ambazo haziingiliani wala kupingana. Ikiwa umetimiza masharti ya kwenda Hijjah nawe unadaiwa Swawm unaweza kwenda Hijjah na utakaporudi nyumbani utaanza kulipa deni la funga kwa siku unazodaiwa za Ramadhwaan bila mushkila wala tatizo lolote.

 

Bonyeza kiungo kifuatacho kupata maelezo ziada:

 

Fataawaa: Kulipa Swawm Na Kafara

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share