21-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kuwalipia Zakaatul-Fitwr Wafanyakazi

 

 

Kuwalipia Zakaatul-Fitwr Wafanyakazi

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Tuna kiwanda na shamba ambamo kuna wafanyakazi wanaolipwa mishahara. Je tuwalipe Zakaatul-Fitwr au wajilipe wenyewe?

 

JIBU:

 

Wafanyakazi ambao wanalipwa mishahara kwa kibarua chao katika kiwanda au shamba wanapaswa kujilipia wenyewe Zakaatul-Fitwr kwa sababu hukmu ya asili ni kwamba imewajibika kwako. (Hivyo hupasi wewe kuwalipia)

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (9/372)]

 

 

 

Share