Inafaa Kuwapa Zakaah Ndugu?

Inafaa Kuwapa Zakaah Ndugu?

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Asalam Aleikum ndugu zangu,
 
Allah Barik In Shaa Allah  kwa juhudi zenu.  Mimi swala langu nila zakat nataka kujua kama ninavyo fanya ni sawa katika dini yetu ya kiislamu.  Zakat yangu huwapa dada zangu wawili mmoja ni mkubwa wangu sana lakini hajaolewa na wapili ni mdogo wangu ana watoto sabaa Mola amuwekee na mume hana kazi nataka kujua kama ya faa mimi kuwapa zakat kwa vile ni familia yangu mimi huwa nyoshea niwezapo si zakat tu peke yake.  Shukran In Shaa Allah nasubiri jawabu yenu ahsantum jazakallah kher

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Hukufafanua kama umekusudia Zakaatul-Fitwr au Zakaah ya Mali inayofika mwaka.

 

 

Hata hivyo kwa hali zote inafaa kuwapa ndugu zako Zakaah ikiwa hali zao ni wenye kuhitaji. Kufanya hivyo utakuwa umefanya mambo mawili pamoja; utatimiza fardhi yako na pia utatimiza amri ya kuunga ukoo na jamaa. Na swadqah unayoitoa kwa jamaa wenyewe kuhitaji ni bora zaidi kuliko kumpa mtu wa nje hii ni kutokana na kauli ya   Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swadaqah zenu kwa jamaa ni Swadaqah na pia ni kuunga ukoo)) 

 

Kwa faida zaidi soma Fataawaa katika viungo vifuatavyo:

 

 

Kutoa Zakaah (Zakaatul-Maal)

 

Fataawaa: Za Zakaatul-Fitwr

Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Za Zakaatul-Fitwr

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share