Jimai: Kutokwa na Manii kwa Matamanio Ramadhwaan Bila Ya Kitendo Cha Ndoa Nini Hukmu Yake

SWALI:

Ikiwa nimiamka asubuhi na swaum na nimeshikwa na matamanio ya kumwingilia mke lakini hatukufanya tendo la ndoa ila nimetokwa na manii..Jee naruhusiwa kuendelea na swaum ama inatakiwa vipi?

 


JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. Mtu akiwa amefunga anaweza kumkumbatia mkewe, akambusu lakini inabidi awe ni mtu anayeweza kuyazuilia matamanio yake asiende zaidi ya hapo.

Jibu ni kwamba ikiwa  utamtamani mkeo mchana wa Ramadhaan na katika kufanya hivyo ukatokwa na manii basi Swawm yako itakuwa imevunjika na hufai kula wala kunywa.

 Hiyo ni kusema ni kuwa unatakiwa ujizuilie na vitu hivyo mpaka Magharibi.

Baada ya Ramadhaan inafaa ulipe siku hiyo moja lakini hutakuwa na kafara yoyote. Pamoja na kulipa siku moja unafaa urudi kwa Allaah Aliyetukuka, uombe maghfira, ujute na uweke azma ya kutorudia tena dhambi

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share