Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga

Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga

 

 

Vipimo

Mchele wa basmati - 3 Vikombe

Dengu - 2 vikombe

Viazi - 3 vikubwa

Kitunguu - 2 kubwa

Nyanya - 2

Pilipili mbichi kubwa - 3

Pilipilimanga - ½ kijiko cha chai

Garama Masala (bizari mchanganyiko) -1 kijiko cha chai

Supu ya vidonge (stock cubes) - 2 vidonge

Chumvi - kiasi

Mafuta - ¼ kikombe

Zaafarani - 1 kijiko cha chai

 

 

Samaki wa kukaanga

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Dengu kama sio za tayari kwenye kopo, roweka na zichemshe hadi ziwive

 

Masala Ya Dengu:

  1. Zaafarani – iroweke katika maji ya dafu dafu (warm) ya chini ya robo kikombe weka kando.
  2. Osha mchele, roweka.
  3. Menya viazi na vitunguu, katakata vitunguu, na nyanya , weka kando.
  4. Katakata viazi  vipande vidogo vidogo kwa umbo la mchemraba (cubes).
  5. Katika sufuria tia mafuta yakipata moto, tia viazi ukaange kidogo kwa moto mdogo mdogo hadi kukaribia kuwiva, toa weka kando.
  6. Kaanga vitunguu hadi vigeuka rangi ya hudhurungi isiyokoza (light brown) kisha tia nyanya ukaange kidogo.
  7. Tia vidonge vya supu (stock cubes) uvivuruge katika mchanganyiko, katakata pilipili mbichi kwa urefu tia, uendelee kukakaanga. Tia bizari, chumvi.
  8. Zima moto, changanya dengu na viazi katika mchanganyiko huo.

  

 

Wali:

  1. Chemsha mchele kama kawaida ya kupika wali mweupe, kiini kiwe kimewiva nusu yake.
  2. Chuja maji kisha changanya katika mchanganyiko wa dengu.
  3. Nyunyizia zaafarani, uchanganye wali na mchanganyiko kidogo tu.
  4. Funika acha uive katika mtoto mdogo mdogo au tia katika oveni hadi uive kama kawaida ya kupika wali.
  5. Pakua katiha sahani na tolea na samaki yoyote wa kukaanga.

 

Kidokezo:

Ukipenda punguza mchanganyiko wa dengu kama vijiko viwili vya supu kwa ajili ya kujaza katika samaki.

 

 

Share