Samaki Nguru Kwa Rojo La Koliflawa

Samaki Nguru Kwa Rojo La Koliflawa

 

Vipimo 

        

Samaki nguru (king fish) - 6 Vipande au wazima

Kitunguu saumu (thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu

Chumvi - kiasi

Pilipili nyekundu  ya unga - 2 vijiko vya chai

Bizari ya samaki (au yoyote upendayo) - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 3 vijiko vya supu

Koliflawa - ½ 

Vitunguu - 3

Nyanya - 4

Nyanya kopo - 2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi -  3

Chumvi - kiasi

Bizari ya mchuzi

Mafuta ya Kupikia - Kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Kaanga samaki kwa bizari ya samaki, chumvi na ndimu.
  2. Chambua koliflawa katakata.
  3. Katika karai, tia mafuta vijiko viwili vya supu, kaanga vitunguu vilokatwakatwa hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown) isiyokoza.
  4. Katakata nyanya, pilipilii mbichi, kaanga pamoja na vitunguu.
  5. Tia nyanya kopo, chumvi, bizari ya mchuzi changanya vizuri.
  6. Tia maji kiasi robo kikombe uchanganye iwe sosi.
  7. Tia koliflawa uache kidogo tu katika moto
  8. Panga samaki katika chombo au sahani ya kupakulia.
  9. Mwagia sosi juu yake ikiwa tayari kuliwa kwa wali au mkate.

Kidokezo: 

 

Samaki ukipenda mchome (bake/grill) katike oveni. Ikiwa utamchoma (bake) unaweza kumchoma pamoja na koliflawa.

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

Share