Muda Wa Kurudi Katika Dini

SWALI:

Asalaam  Alaikum  Warahmatulhaahi  Wabarakaatuhu,  mimi  sijambo [ Al Hamdulillaah] kama  nanyi  hamjambo viongozi  wetu wa Dini  ya kweli basi ni kheri. Naomba msaada mnijibu

Mtu  aliyesilim  kutoka kwenye Dini  ya  kweli  kisha  baada  ya  muda  fulani  akataka kurudi  anaruhusiwa?


 

JIBU:

AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

Mtu ambaye alikuwa ni Muislamu kisha akaritadi anaweza kurudi katika Dini anapoona kuwa amefanya makosa. Na jambo hili lilitokea wakati wa Abu Bakar Asw-Swiddiyq (Radhiya-Allaahu 'anhu) ambapo Waarabu waliritadi na baadae wakarudi katika Dini yao ya asili. Na ni makosa makubwa sana kwa mtu kufanya kitendo hicho cha kuingia na kutoka katika Dini kwa dhihaka au istihzai. Lakini likifanywa mara nyingi litamletea matatizo makubwa sana mtu mwenyewe kwani litamuingiza katika ukafiri. Allaah Anasema:

“Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Allaah Hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia” (4: 137).

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share