Mshirika Wa Chumba Anapiga Muziki Sana Je Nami Niache Qur-aan Isome Pamoja na Muziki?

 

SWALI:

 

Assalaamu aleykum wa rahmatullahi taala wa barakaatuhu. 

Alhamdulillah kwa utukufu wa Allah, kutuwezesha kua na website inayotusaidia kiimani na ibaada za kiislam. Nakushkuruni maulamaa wa ALHIDAAYA kwa kua mnatusaidia sana hasa sisi tulioko mbali na miongozo ya wazee katika nchi hizi za kitwaaghut.

Mimi ni mwanafunzi wa college nchini marakani. Room mate wangu ananisumbua sana na mziki. Anapiga miziki misauti mikubwa. Inaniathiri kiasi kwamba hata nikisali sina khushu'u. Nimedownload adhana kutoka islamic finder, ikiadhini adhana nahisi bora niizime kuliko kuiacha na huku miziki inapigwa kwani itakua naikashshif adhana. Pia nikiwa naskiliza Qur-an nafanya hivyo ili kuitukuza Qur-an. Jee nnavyofanya ni sawa au inakua naiopress dini yangu kwa ajili ya kafiri? Ni lipi bora kwangu kufanya nnapokua katika ibada zangu na hali hii?

Natanguliza shukrani zangu kwenu, jazaakumullahu khairun.

 


 

JIBU:

AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mweka muziki mnayekaa naye. Hakika hilo unalopata wewe ni kero tena kubwa sana lakini katika dunia hii kila Muislamu anapata mitihani kwa njia yake. Na huo ni aina ya mtihani ambao Allaah Aliyetukuka Ametaka upate ili kukuza Imani yako. Tufahamu kuwa anayependwa na Allaah ndiye mwenye kupewa mitihani. Allaah Aliyetukuka Anatueleza kuhusu mitihani pale Aliposema:

 

Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? Hakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Allaah Atawatambulisha walio wa kweli na Atawatambulisha walio waongo” (29: 2 – 3). Ikiwa mitihani haina budi kwa Muislamu, basi ni lazima tujipambe na tabia ya subira na uvumilivu kukabiliana na mitihani kama hiyo.

 

Ni katika hekima saa nyengine ukanyamaza bila kusema chochote na wakati mwengine kumfanyia wema anayekuudhi. Kwa ajili ya hiyo ndio Allaah Aliyetukuka Akatuambia:

Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Allaah na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu? Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa” (41: 33 – 35).

Ni katika wema kuzungumza naye vizuri, ikiwa una tunu yoyote ukampatia na InshaAllaah Allaah Atambadilisha na hata usijue kama mlikuwa na utesi wa aina yoyote ule. Lakini linapatikana kwa uvumilivu pekee.

Ikiwa hakuwa ni mwenye kujirekebisha hata baada ya kuzungumza naye kwa njia nzuri basi itabidi uende kwa idara ya chuo ili upeleke malalamishi yako kwa kumkanya au wakuhamishe chumba chengine. Mara nyingi katika nchi kama hizo unazosoma idara huwa inatoa kipaumbele kurekebisha hayo kwa kila mtu ana haki ya kupata utulivu kwa kutoghasiwa.

Usiwe ni mwenye kuchukua hatua ya kutia Qur-aan kwani utakuwa unaidunisha na kumpatia nguvu mnaekaa naye. Kisha tufahamu kuwa ikiwa utatia kuwa itabidi uwe ni mwenye kuisikiliza. Na kufanya hivyo pia haitaleta natija nzuri kwa kuueleza Uislamu kwa wasio Waislamu.

Tunakutakia kila la kheri na fanaka katika hilo.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share