Wakati Uliopotea

 

Wakati Uliopotea

 

Imefasiriwa na Ukht Haliymah ‘Abdullaah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Anasema Hasan Al-Baswriy:

 

‘Nimewafikia Watu alikuwa mmoja wao ni bakhili kwa umri wake kuliko dirham.’’

 

Mwanangu mdogo tangu jana jioni Afya yake si nzuri… Niliporudi nyumbani jioni ya leo kutoka kazini niliamua kumpeleka Hospitali… japo nimechoka ila uchovu kwa ajili ya mwanangu ni raha.

 

Nikambeba nikaenda naye… Walikuwa wenye kusubiri ni wengi… Huenda tukachelewa zaidi ya saa… Nikachukua namba ya kuingia kwa Daktari nikaelekea sehemu ya kukaa katika chumba cha kusubiria.

 

Nyuso ni nyingi… wapo wadogo na wakubwa… Ukimya umewafunika wote. Kunapatikana vijitabu vidogo vya kiupitisha muda waliojitolea baadhi ya ndugu.

 

Nikawatupia jicho waliohudhuria… baadhi wamefumba macho yote mawili hujui wanachofikiria….

Mwengine anawatazama wote…. Wengine utawahisi nyusoni mwao  wasiwasi na uchovu wa kusubiri.

 

Inapita ukimya mkubwa… Sauti ya mwenye kunadi… namba kadhaa… furaha katika uso wa aliyeitwa… anaondoka kwa hatua za haraka… kisha unarejea ukimya kwa wote.

 

Nikapiga macho kwa kijana katika umri wa kati hajali yaliyo pembeni mwake... pamoja naye ana Mas-hafu ndogo ya mfukoni... anasoma ndani yake… hanyanyui macho… nikamtazama wala sikufikiria hali yake sana… lakini nilipozidi kumtazama zaidi ya saa nzima ikageuka kutazama kwangu kwenda katika fikra nzito kuhusu namna ya maisha yake na kuhifadhi kwake wakati.

 

Saa nzima katika umri wangu kitu gani nimefaidika nami niko na faragha bila kazi… bali kusubiri yenye kuchosha.

 

Anaadhini Muadhin kwa Swala ya Maghrib… tunaondoka kuiendea Swalah katika sehemu ya kuswalia Hospitalini… nikajaribu kuwa karibu na yule kijana baada ya kumalizwa Swalah, nikawa naye na nikamfahamisha moja kwa moja nilivyostaajabishwa na kuhifadhi kwake wakati.

 

Ikawa mazungumzo yake yanakazia kuhusu wakati mwingi tunaoupoteza ambao hatufaidiki nao; masiku ya umri wetu yanamalizika bila ya kuhisi au kujutia…

 

Akasema… amechukua Mas-hafu ya Mfukoni tangu mwaka mmoja pindi alipohimizwa na rafiki kuhusu kuhifadhi wakati.

 

Akanifahamisha… kwamba yeye anasoma katika wakati ambao hawafaidiki nao wengi zaidi kuliko anavyosoma Msikitini au nyumbani bali kisomo katika Mas-hafu ni ziada katika ujira Allaah Akipenda, pia inamuondolea uchovu na khofu…

 

Akaongezea msimulizi wangu huku akisema kwamba yeye sasa yupo katika sehemu ya kusubiria karibu saa na nusu….

 

Akaniuliza…

 

Wakati gani utapata saa na nusu ili Usome Qur-aan…

 

Nikazingatia… nyakati ngapi zinakwenda bure… ni fursa ngapi katika maisha yako zinapita wala huhesabu hesabu…

 

Bali ni ni miezi mingapi inakupita bila kusoma Qur-aan…

 

Nikavuta kutazama… nikajikuta ninajihesabu na wakati sinao mikononi mwangu… kitu gani nasubiri?.

 

Ikakata fikra zangu sauti ya mwenye kunadi… nikamwendea Daktari.

 

Nataka kuhakikisha jambo sasa.

 

Baada ya kutoka Hospitali… nikaelekea duka la vitabu... nikanunua Mas-hafu ndogo...

 

Nikaamua kuhifadhi wakati wangu… nikafikiri huku naweka mfukoni.

 

Ni watu wangapi watafanya hivyo…

 

Na ni ujira ngapi mwingi utakuwa kwa mwenye kulielekeza hilo…

 

 

WabiLlaahi At-Tawfiyq.

 

 

 

 

Share