'Iyd Mubaarak
‘Abdallaah Bin Eifan
(Jeddah, Saudi Arabia)
(1) Allaahu Akbar Kabira, Walhamdulaahi Kathira,
Tunaomba maghfira, na maisha yalobora,
Na dini ipo imara, inapepea bendera,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(2) Kufunga Sita ni bora, kutimiza msafara,
Itupandishe mnara, juu tuzidi kung’ara,
Itufundishe subira, na kupunguza hasira,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(3) Wavaao matambara, Mungu Awape sitara,
Awaepushe izara, Mungu Anajua bora,
Dunia ipo duwara, faida au hasara,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(4) Tukumbuke kila mara, mauti kwenye fikira,
Tukumbukeni harara, ya moto huko akhera,
Tuacheni maskhara, dunia tutaigura,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(5) Tuacheni kuzurura, watu kwenda kuwapora,
Ni tabia ya Wakora, wenye mengi ya madhara,
Kheri twende muhadhara, Mungu Atupe ujira,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(6) Wafanyao biashara, toa zaka ni tohara,
Ugawe kwa mafukara, Ibarikiwe tijara,
Hio iwe ndio dira, dira ya yako idara,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(7) Mayahudi na Nasara, wanarusha makombora,
Hakika wanatuzira, inawasumbua ghera,
Tutawanyoa vipara, tuzidi kuwazingira,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(8) Onyesha Yako Kudura, Muumba Mwenye Busara,
Waangamize papara, wafe mbele ya hadhara,
Wafe waanze kufura, kufura kama hamira,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
(9) Hapa mwisho wa kuchora, pengine ninawakera,
Beti tisa ni ishara, kuwa nimetia fora,
Nipeni yangu bakora, niivuke barabara,
Iddi Mbaraka Hongera, Kumbuka na Mafukara.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha