Kababu Za Nyama Ya Kuku Ya Kusaga

Kababu Za Nyama Ya Kuku Ya Kusaga 

Vipimo

Nyama ya kuku ya kusaga - 1 kilo

Kitunguu saumu(thomu) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

*Bizari ya Kababu (chaplin Kabab masala) - ½ paketi

Kitunguu kilichokatwakatwa (chopped) - 1

Kotmiri (coriander leaves) - ½ kikombe

Chumvi - kiasi

Mafuta - ¼ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya nyama ya kuku pamoja na viungo vyote katika bakuli.
  2. Fanya madonge shape ya duara kama picha weka kando.
  3. Paka mafuta treya utakayotumia kupikia katika oveni, kisha zipange kababu.
  4. Nyunyizia mafuta yaliyobakia kisha choma (grill) kwa moto wa kiasi na ugeuze kababu zinapowiva upande mmoja.
  5. Epua zikiwa tayari kuliwa na saladi, wali au mikate

Kidokezo:

*Bizari unaweza kutumia zozote upendazo ila hiyo ya ‘Chaplin’ inayouzwa tayari katika paketi inaleta ladha nzuri katika kababu aina hii.

 

 

 

 

 

 

Share