Zingatio La Wiki - Sio Kila Kitu Kinaonekana
‘Abdun-Naaswir Hikmany
Dunia ni tamu na kawaida ya mwanaadamu kupenda mazuri mno. Hujitahidi kadiri ya juhudi zake kukusanya yale ayaonayo kuwa ni yenye kufurahisha nafsi yake. Hutafuta yale yenye laghai na anasa - 'material world'.
Waislamu walio wengi kabisa wanatamka shahaadah ya kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ni Mmoja na Ndiye Apaswaye kuabudiwa pamoja na kutiiwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kikomo cha wengi kinamalizia hapa kwenye kauli tu. Matendo
{{Ambao wanamuogopa Mola wao (hata) wanapokuwa faraghani, na pia hukiogopa Qiyaama.}} [21:49]
Taariykh yatufunza kwamba Waislamu hapo kale walilelewa kwenye Tawhiyd ya kumuamini Allaah pamoja na Malaika, Mitume, Vitabu, Siku ya Mwisho, Qadar kheri na shari. Kwa wakati wa sasa ni Kitabu cha Qur-aan pekee ndicho kilicho mbele ya macho yetu. Vilivyobaki vyote vinabaki kuwa nyuma ya pazia 'ghaibu'.
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘Anhu): amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba:
"Iymaan ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Kukutana Kwake (Siku ya Qiyaamah), na Mitume Wake na kuamini ufufuo wa Siku ya Mwisho." (Imepokewa na Shaykhaan)
Kukosa kuamini moja ya nguzo za iymaan, kunapelekea kutoamini ghaibu. Hivyo, kuanguka kwa iymaan ya ghaibu kutasababisha kuondoka iymaan ya kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Yupo.
Ni ghaibu hii inayomfanya mwanaadamu na hata Muislamu kutotilia mkazo kuutafuta ukweli halisi wa Uislamu, ghaibu ndiko kunakomfanya Muislamu kutotenda mema kwa lengo la kupata ridhaa ya Allaah. Thawabu wala dhambi hazioni mtu, Malaika wanaoandika mema na maovu nani anayewaona? Haya yote yapo kwenye ghaibu. Muislamu anatakiwa kuamini hii ghaibu bila ya mjadala. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anatuambia:
{{Tendeni mambo (mazuri). Mwenyezi Mungu Atayaona mambo yenu hayo na Mtume Wake na Waislamu. Na mtarudishwa kwa Mjuzi wa siri na dhahiri; Naye Atakwambieni (yote) mliyokuwa mkiyatenda.}} [9:105]
Apambanue Muislamu juu ya kukosa kwake iymaan ya ghaibu na kuirudisha nyuma akili kabla ya kuwepo kwake; yeye alikuwa ni nani? Nani aliyemhifadhi ndani ya tumbo la mama kwa miezi tisa? Hivyo, ghaibu ni wajibu kuiamini na kwamba yapo mambo nyuma ya macho yetu yanatokea au yapo tayari kutokea.
Kukosekana kwa iymaan ya ghaibu ndani ya nafsi ya Muislamu ndio kwamfanya awache himma ya kutenda mema. Ni sababu hii inayowafanya vijana walio wengi kujishughulisha mno na ratiba za mipira inayokula muda wa Waislamu. Nao kina dada kutilia mkazo urembo, mikusanyiko ya haramu na kutembea kwao utupu kunatokana na kukosa kwao kuamini ghaibu.
Basi na aangalie Muislamu alivyoumbwa, chakula chake kinavyoyayushwa na kugaiwa sehemu mbali mbali. Vitamini, damu, madini, sukari, chumvi, mafuta na vyengineo; vyote vinapelekwa na kuhifadhiwa sehemu zake maalum. Atupe jicho
{{Naye ndiye Aliyeziumba mbingu na ardhi kwa haki. Na wakati Anaposema (kuliambia jambo): "Kuwa," basi huwa… Mjuzi wa ya siri na dhahiri…}} [6:73]
Basi ni mengi yaliyopo Mkononi Mwako yaa Allaah! Namna tutakavyojifunza katu hatutafikia chembe ya 'ilmu Yako. Hivyo, tunatamka
{{Wewe Umetakasika na kuwa na mshirika. Hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


