Skip navigation.
Home kabah

Kulipiwa Riba Ya Mkopo Wa Masomo Na Serikali Isiyo Ya Kiislamu Inafaa?

SWALI

Assalam a'laykum

Nilikuwa na swali ambao ningependa kuuliza. Swali lenyewe ni jee ni inafaa mtu kuchukuwa mkopo ambao una ribaa ndani yake lakini mtu mwengine asiekuwa Muislamu alipie ile riba sio yeye? Sababu ya kuuliza swala hili ni ya kwamba katika nchi niliyokuwepo inajulikana ya kuwa wanafunzi wanapewa mikopo kupita program maalum mpaka watakapo maliza masomo. Pindi watakapo maliza au kuacha masomo, wanakuwa wanahitajika kulipa pesa zote zile ambazo wamezikopa kwa miezi sita na miezi hiyo ikishapita basi unawekewa interest katika mkopo wako. Naweza kusema ya kwamba hawezekani kabisa kwa mwanafunzi kulipa pesa zote zile kwa miezi sita kwa sababu (a) hela zinakuwa nyingi na (b) saa nyingine mtu hajapata hata kazi kwa kipindi hicho.

Hata hivyo, nimekuja kuchuwa ya kwamba unaweza kuomba kupewa muda kidogo bila ya kulipishwa interest ukitowa dharura. Na kwa kipindi hicho serikali inakuwa inakulipia ribaa zako. Na zaidi, nimegunduwa ya kwamba katika kipindi ambacho uko shule mkopo wako unawekwa katika interest-free status, na wamesema hii ina maana ya kwamba hutolipa ribaa alimradi uko shule na serikali itaendelea kukulipa ribaa yako mpaka ukimaliza shule.

Kwa hiyo maswala langu ni jee inafaa kuchukuwa mkopo ambao wewe hulipii ribaa lakini mtu mwingine analipa? Kwa sababu mimi ninaweza kuepukana na kuilipa hiyo ribaa baadae kwa kufanya kazi na kulipa deni wakati wa kufungwa shule. NA zilikifunguliwa itabidi nichukuwe mkopo mwingine kwa sababu sina uwezo wa kulipa fee yote. Kwa hiyo inshaaAllah sitolipia pesa za ziyada isipokuwa zile nilizozikopa tu.

Jazakum Allah Khayran


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kukopa kwa ajili ya kusoma na kulipa pamoja na riba. Allaah Aliyetukuka Ameharibisha riba na kuiwekea vikwazo kwa watu kutoendea. Jambo lolote ambalo linaikuza riba limeharamishwa. Kuchukua mkopo na mwengine asiyekuwa Muislamu ni kuipa nguvu shughuli na jambo hilo la riba hivyo kuziimarisha taasisi hizo kwa njia moja au nyingine. Ikiwezekana kama kuna njia nyingine ni bora utumie njia zisizokuwa za riba.

Muislamu anatakiwa afanye juhudi za hali ya juu kujiepusha kwa njia zote na riba. Hakuna nchi ambayo inawalazimisha raia zake kuchukua mkopo wa riba kutoka kwa serikali. Ni mwanafunzi kukosa uwezo ndio huwa anatafuta njia za kuweza kujikimu kimaisha na kimasomo. Muislamu anafaa atafute njia zote ili kuweza kujitoa katika dhambi la kukopa kwa kulipa pamoja na riba. Ikiwa amekosa njia kabisa na masomo anayosoma ni miongoni mwa masomo ambayo yatausaidia Ummah huu wetu basi anaweza kuchukua na huku amechukia.

Na Allaah Anajua zaidi