Kuvaa Saa Mkono Wa Kushoto Kuna Ubaya?

 

 

Kuvaa Saa Mkono Wa Kushoto Kuna Ubaya?

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam Alaykum, Amma baad, naomba nifahamishwe je kuvaa saa mkono wa kushoto pana ubaya?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ni jambo linaloeleweka kuwa ni katika maadili ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alikuwa akitumia mkono wa kulia kwa mambo mazuri na wa kushoto kwa vitu vibaya. Mfano akitawadha akianza upande wa kulia, akiingia Msikitini pia akitumia mguu wa kulia. Ama alipokuwa akiingia chooni akitumia mguu wa kushoto na kutamba akitumia mkono wa kushoto.

 

Anasema Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa): “Alikuwa akipenda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuanza kuutumia mkono wa kulia wakati akivaa viatu vyake, na kujitana kwake, na katika kujitwaharisha kwake, na katika kutenda mambo yake yote.” [Al-Bukhaariy Na Muslim].

 

‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu  kuvaa saa mkono wa kushoto.

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) ameulizwa akajibu: “Hakuna ubaya kuvaa saa mkono wa kulia au kushoto, au kuvaa pete kwa sababu imepatikana dalili kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivaa pete kidole chake cha kulia na alivaa pia kushoto [Fataawa  Islaamiyyah (4/255)]

 

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah wamefutu:  “Jambo lina wasaa na inategemea wepesi wa mtu kuitumia, kwake ikiwa mkono wa kulia au kushoto”  [Fatwa namba 9584]

 

 

Imaam Albaaniy ameona kuwa ni kuivaa mkono wa kulia kwa sababu ya dalili kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipendelea zaidi kutumia mkono wa kulia katika mambo kadhaa na pia kuivaa mkono wa kushoto ni kujipeusha kuwafuata makafiri. [Fataawa Al-Madiynah (58) – Masaa’il ‘Ilmiyyah]

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share