Mie Simo
‘Abdun-Naaswir Hikmany
Shukurani zote ni za kwake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Aliyetujaalia kuwa miongoni mwa wanaoitamka kalimah. Hatuna budi kuelekeza nia, kauli na vitendo vyetu vyote kwa ajili Yake Muumba Pekee. Yote mazuri tuyatendayo yanatokana na Mwenyezi Mungu na mabaya yote yanatokana na kasoro zetu.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ndiye Ajuaye yaliyomo ndani ya nafsi zetu na wala sisi hatujui yaliyomo ndani ya nafsi Yake. Tunakuomba Mola wetu Mlezi utujaalie kheri kwa wanayotudhania, usituchukulie makosa kwa yanayosemwa juu yetu na utusamehe kwa madhambi ambayo hawayafahamu.
Amma ba'ad:
Kuna mchezo maarufu miongoni mwa watoto ambao huchezwa
{{Na Shaytwaan atasema itakapokatwa hukumu (ya wema kwenda Peponi na wabaya kwenda Motoni; atawaambia wale waasi watakaomng'ang'ania): "Mwenyezi Mungu Alikuahidini ahadi ya kweli (na leo Ameitimiza), nami nilikuahidini; lakini sikukutimizieni. Wala sikuwa na mamlaka juu yenu (ya kukulazimisheni kunifuata); isipokuwa nilikuiteni tu, nanyi mkaniitika. Basi msinilaumu, bali jilaumuni wenyewe siwezi kukusaidieni wala nyinyi hamuwezi kunisaidia. Hakika mimi nilikataa kunishirikisha kwenu toka zamani." Kwa yakini madhalimu watakuwa na adhabu iumizayo.}} [Ibraahiym: 22]
Ibilisi amechukua ahadi mbele ya Muumba kwa kusema kwamba atawapotosha wanaadamu ili wasiione nuru ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala), waache kutekeleza maamrisho ya Mtume Wake pamoja na kutofuata njia sahihi ya diyn ya Kiislamu.
Atawakalia mbele
Rafiki mwema ni yule ambaye atakufaa duniani na akhera. Huyu si mwengine bali ni ndugu yako wa Kiislamu asiyependa ukhasirike:
{{Isipokuwa wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri, na wakausiana (kufuata) haki na wakausiana (kushikamana) na subira (kustahamiliana).}} [Al-'Asr: 3]
Munakutana kwenye madarasa mukishindana kuisaka elimu ya Kiislamu pamoja na kusaidiana kutekeleza yaliyoamrishwa na Muumba Mlezi. Tofauti kabisa na Ibilisi pamoja na jeshi lake, ambao wana usuhuba wa kunyunyizia marashi juu ya kichwa tu kama kwenye harusi. Hata ukifika kwako harufu haipo nawe.
Tujitahidi kufuata Qur-aan na Sunnah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwani hizo ndio kinga kuu za kumzuia Ibilisi kutuhadaa.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



asalamu aleikum
asalamu aleikum warahmatullahi wabarakatuh napenda kuwauliza kwamba kama wewe ni islamu waruhusiwa kuingiya kanisani naomba majibu ikiwezekana shukran