Ana Majini Amefanyiwa Matibabu Lakini Hakupona Afanyeje?

 

Ana Majini Amefanyiwa Matibabu Lakini Hakupona Afanyeje?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI

 

Asalamu alaikum warahmatu llah wabarakatu,

 

Nashukuru sana kwa majibu yenu ambayo mnatujibu kupitia mtandao huu. Suala langu ni kwamba, Mimi nina matatizo ya kuugua maradhi ya Majini (mashetani) kwa muda wa mwaka mmoja sasa, nimefanyiwa visomo mara nyingi lakini hadi sasa sijapata nafuu, na maelezo yenu mara nyingi yanaelekea kwenye kujikinga na tatizo, ni njia gani sasa nitayoweza kuitumia ili kuondokana na tatizo hili (dua au visomo vizito zaidi)

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hata hivyo, hukutueleza visomo vyenyewe ulifanyiwa namna gani? Na je, vilikuwa ni kwa njia ya Sunnah au vipi? ‘Alaa kulli haal, unatakiwa kwa wakati huu uwe unajikinga mwenyewe kwa kusoma Qur-aan na nyiradi tofauti.  Bonyeza viungo vifuatavyo utapata maelezo mengi ya kuhusu vipi kujikinga na tiba zake:

 

Naingiliwa Na Majini

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Na kijitabu ambacho kinaweza kukusaidia katika hilo ni Hiswn al-Muslim ambacho kinapatikana hapa:

 

Hiswnul Muslim

 

Mbali na hilo unatakiwa labda ubadilishe anayekusomea na utafute mwengine ambaye anafahamika kwa elimu, ujuzi wake na ucha wa Allaah. Na kisomo hicho kinatakiwa kikaririwe kila siku kwa muda utakaopendekezwa na Shaykh mwenyewe. Hakuna maradhi yasiyokuwa na dawa na wala usichoke kufanya dawa inayokubaliwa kisheria.

 

Tunakuombea kwa Allaah Aliyetukuka Akuponyeshe na maradhi yako.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share