Wanawake Wepi Ambao Wanaume Waliomiliki Mikono Yao Ya Kuume Wameruhusiwa Kuwaingilia?

SWALI LA KWANZA

 

 

Sifa njema zote ni za ALLAH [SW], Kheri na baraka zake zimfikiye kipenzi chake Nuru yetu na muombezi wetu MTUME [SAW], Maswahaba na watangulizi wema hadi ya~Umulhesabu. ALLAH [s.w] awajaze kheri zake wote mnao husika na Mtandao wa AL~HIDAAYA kwani ni Nusura kwa Umma huu wa MUHAMMAD [SAW].

 

QURAN 23:6 ALLAH anasema ruhusa kuwaingilia wanawake tulio waoa na wale tuliowamiliki kwa mikono yetu ya kulia kwao hatuta laumiwa. Wanawake hao ni wepi?

 

ALLAH awalipe kheri, Insha~ALLAH.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu wanaomilkiwa na mikono yetu ya kuume.

 

Ama inayomiliki mikono ya kuume ni wale watumwa wa kike walioshikwa na Waislamu katika vita vya Jihaad. Kuna fadhila ya kuwaacha huru wanawake hawa na thawabu ya kufanya hivyo ni nyingi mbele ya Allaah Aliyetukuka. Na ikiwa utamuoa basi itakuwa ni kheri kama ilivyo katika Suratun Nisaa', Aayah ya 3. Na hasa Uislamu umeweka mikakati mizuri ya kuweza kuwakomboa watumwa, kulipa fidia au wao wenyewe kujikomboa kwa mapatano baina yenu. Kwa hiyo, hapa Allaah Aliyetukuka Ametoa ruhusa kwa njia mbili ya kuweza kujitosheleza kwa wanawake, kwa kufanya mapenzi na mkeo wa halali na kufanya hilo na watumwa walio chini ya mmoja wenu. Kufanya moja katika ya hayo mawili hakuna lawama.

 

Maelezo zaidi katika viungo vifuatavyo:

 

 

Waliomiliki Mikono Yao Ya Kiume Ina Maana Inafaa Kufanya Mapenzi Na Wafanya Kazi Wa Nyumbani?

 

House Girl Sio Wale Waliomiliki Mikono Yetu Ya Kuume

 

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share